Russia yadaiwa huenda ikawapiga risasi wanajeshi wake wanaokimbia vita Ukraine

Rais wa Russia Vladimir Putin

Russia inawezekana iko tayari kuwapiga risasi wanajeshi wanaondoka katika jeshi au kukimbia vita nchini Ukraine, kulingana na taarifa mpya za Wizara ya Ulinzi ya Uingereza juu ya vita vya uvamizi wa Russia nchini Ukraine.

“Kutokana na kushuka morali na kutotaka kupigana, majeshi ya Russia pengine yameanza kupeleka “wanajeshi wa kuwazuia” au “vikosi vya kuwazuia,” taarifa mpya za kijasusi zilisema. Vikosi hivi vinatishia kuwapiga risasi wanajeshi wao wenyewe watakao rudi nyuma wakiwa vitani ili kulazimisha mashambulizi na imetumiwa kama hivyo katika vita vya zamani na majeshi ya Russia.”

Hivi karibuni majenerali wa Russia inaelekea walitaka makamanda wao kutumia silaha dhidi ya wanaokimbia vita, ikiwemo uwezekano wa kuamrisha kuuawa kwa wanaokimbia baada ya onyo kutolewa,” Wizara ya Ulinzi ilisema, “Majenerali pia inawezekana walitaka kuendelea kuimarisha ulinzi wa maeneo hata kama itamaanisha kifo.”

Mbinu hiyo ya kuwapiga risasi wanajeshi wao wanaokimbia vita, wizara imesema, “inawezekana inaainisha utendaji duni, morali ya chini na ukosefu wa nidhamu kwa jeshi la Russia.”

Siku ya Ijumaa Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken alikutana na wenzake kadhaa wa kimataifa – Waziri wa Mambo ya Nje wa Ufaransa Catherine Colonna, Waziri wa Mambo ya Nje wa Ujerumani Annalena Baerbock, Waziri wa Mambo ya Nje wa Uingereza James Cleverly – nchini Ujerumani kujadili “ushirikiano unaoendelea na mataifa ya upande wa pili wa bahari ya Atlantic juu ya masuala kadhaa muhimu, ikiwemo kuendelea kuiunga mkono Ukraine wakati ikikabiliana na ukatili wa vita vya uvamizi vya Russia” na “msaada wa kijeshi wa Iran kwa Russia na msako mkali na kuwakandamiza wananchi wa Iran,” kulingana na taarifa ya Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani.

Wakati huohuo, Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy alipongeza majeshi yake Alhamisi wakati nchi hiyo ikiadhimisha siku maalum maarufu kama Day of Missile Troops and Artillery and the Day of Engineering Troops

“Makombora ya Ukraine yamekuwa ni bora sana katika bara la Ulaya na yenye nguvu kabisa duniani,” Zelenskyy alisema.

“Siku zote itakuwa hivyo. Licha ya ubora wa kombora la adui – kwa idadi – wapiganaji wetu wanatoa matokeo bora zaidi. Faida ya wapiganaji wetu ni ubora wake – maarifa, umahiri, imani yao kwa nchi yetu.