Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Desemba 26, 2024 Local time: 00:24

Ukraine yaomba Russia iondolewe kwenye taasisi za kimataifa


Russia wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy kwenye picha ya maktaba.
Russia wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy kwenye picha ya maktaba.

Maafisa wa Ukraine Jumanne wameomba Russia iondolewe kwenye taasisi za kimataifa, baada ya wanajeshi wake kufanya mashambulizi kwenye miundombinu muhimu katika miji kadhaa ya Ukraine.

Msemaji wa wizara ya mambo ya kigeni wa Russia Oleg Mikolenko amesema kwamba Russia inafaa kuondolewa kwenye uanachama wa mataifa ya G-20, huku akiombia kufutiliwa mbali kwa mwaliko wa rais wa Russia Vladimir Putin kwenye mkutano wa kundi hilo mwezi huu nchini Indonesia.

Nikolenko kupitia ujumbe wa twitter amesema kwamba Putin aliamuru kushambuliwa kwa raia pamoja na miundombinu ya nishati, na kwa hivyo mikono yake imejaa damu na wala hatakiwi kuruhusiwa kuketi meza moja na viongozi wa dunia. Kwenye hotuba yake ya kila siku kwa taifa Jumatatu jioni, rais wa Ukraine Volodymr Zelensky amesema kwamba Russia haitakiwi kupewa nafasi kwenye baraza la usalama la Umoja wa Mataifa.

Jeshi la Ukraine limesema kwamba mashambulizi ya Russia ya Jumatatu yalihusisha zaidi ya makombora 50 ya masafa marefu. Putin amesema kwamba mashambulizi hayo ni kufuatia shambulizi la Ukraine kwenye msafara wa meli wa Russia kwenye bahari ya Black Sea.

XS
SM
MD
LG