Meya wa Kyiv Vitali Klitschko alisema mashambulizi katika mji mkuu yalikata umeme na usambazaji wa maji katika baadhi ya maeneo ya jiji, na kuacha zaidi ya asilimia 80 ya wakaazi wake bila maji ya bomba. Kufikia usiku, idadi hiyo ilipungua hadi asilimia 40.
Katika ujumbe wake wa Twitter, Waziri wa Mambo ya Nje wa Ukraine Dmytro Kuleba alilaani mashambulizi hayo, akiandika:
"Makombora mengine ya Russia yamepiga miundombinu muhimu ya Ukraine. Badala ya kupigana kwenye uwanja wa vita, Russia inapigana na raia. Usihalalishe mashambulizi haya kwa kuyaita 'majibu.' Russia inafanya hivi kwa sababu bado ina makombora na nia ya kuwaua raia wa Ukraine."