“Hatujawahi kukabiliwa na hali kama hii ya vita vya nyuklia tangu Kennedy na mgogoro wa Mokombora ya Cuba,” Biden alisema wakati hafla ya kuchangisha pesa mjini New York kwa ajili ya Kamati ya Kampeni ya Maseneta Wademokrat.
Mwezi Oktoba 1962 Marekani na Umoja wa Sovieti walikaribia kuingia katika vita vya nyuklia baada ya Marekani kupeleka makombora ya balistiki nchini Uturuki na Italia huku Russia ilijibu kwa kuweka makombora kama hayo nchini Cuba.
Rais Biden alisema Rais wa Russia Vladimir Putin, “mtu ambaye na mfahamu vizuri,” hafanyi mzaha anapozungumzia kutumia “silaha za nyuklia au kibaiolojia na kemikali.”
“Sidhani kama kuna kitu kama hicho wakati uwezo wa kutumia kwa urahisi silaha za nyuklia katika harakati za vita na hatuaishia katika silaha hizo,” alisema Biden.
Akizungumza na wafadhili Wademokrat, Biden alisema yeye na maafisa wa Marekani walikuwa bado “wanajaribu kutafuta njia ya kumfanya Putin abadilishe mwelekeo” huko Ukraine.
“Ni wapi atapata njia ya kujitoa?” alisema Biden. “Wapi ataweza kufikia mahali ambapo siyo hatapata fedheha lakini pia akapoteza madaraka makubwa ndani ya Russia?”
Rais alisisitiza kuwa Marekani itaendelea kuiunga mkono Ukraine.