Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Novemba 05, 2024 Local time: 19:44

Vikosi vya Ukraine vyaendelea kukomboa maeneo ya kusini


Wanajeshi wa Ukraine kwenye picha ya maktaba
Wanajeshi wa Ukraine kwenye picha ya maktaba

Vikosi vya Ukraine  Jumatatu vimepiga hatua katika mkoa wa Kherson kusini mwa nchi, wakati vikiendelea kukabiliana na vile vya Russia kuelekea upande wa mashariki katika siku za karibuni.

Maafisa wa Russia wanaoshikilia Kherson wamesema kwamba jeshi la Ukraine limekomboa tena baadhi ya makazi katika mkoa huo. Rais wa Ukraine katika hotuba yake kwa taifa Jumapili usiku, amesema kwamba vikosi vyake vimekomboa makazi ya Arkhanhelski na Myroliubivka. Russia haijasema lolote kufuatia hatua ya Ukraine ya kuchukua tena mji wa Lyman ingawa Jumamosi ilisema kwamba vikosi vyake vinaondoka mjini humo kwa hofu ya kuzingirwa na vikosi vya Ukraine.

Russia iliuteka mji huo mwezi Mei, na tangu wakati huo imekuwa ikiutumia kama kitovu cha kiufundi pamoja na shughuli za usafirishaji, kwenye operesheni kaskazini mwa mkoa wa Donetsk. Kuchukiliwa tena kwa Lyman ni ushindi mkubwa sana kwa vikosi vya Ukraine tangu vilipoingia kwenye mkoa wa Kharkiv kaskazini mashariki mwa nchi mwezi uliopita, na kuvisukuma vikosi vya Russia kelekea kwenye mpaka.

XS
SM
MD
LG