Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Novemba 05, 2024 Local time: 19:29

Baraza la Seneti la Russia lapiga kura ya kuidhinisha mikoa minne ya Ukraine kuwa sehemu ya Russia


Baraza la Seneti la Russia laidhinisha mikoa minne ya Ukraine kuwa sehemu ya Russia, katika kikao chake cha Oktoba 4, 2022. Picha ya Reuters
Baraza la Seneti la Russia laidhinisha mikoa minne ya Ukraine kuwa sehemu ya Russia, katika kikao chake cha Oktoba 4, 2022. Picha ya Reuters

Baraza la Seneti la Russia Jumanne limepiga kura ya kuidhinisha mikoa minne ya Ukraine kuwa sehemu ya Russia, na kusukuma mbele mchakato uliolaniwa na Ukraine na washirika wake wa magharibi.

Hatua ilielezewa na katibu mkuu wa Umoja wa mataifa Antonio Guterres kama “hatari ya kusambaa kwa mzozo” na kwamba mchakato huo hauna nguvu ya kisheria.

Bunge la Russia lilikuwa tayari limeshaidhinisha baada ya Russia kuandaa kura ya maoni katika mikoa minne ya Ukraine inayokaliwa na wanajeshi wa Russia.

Ukraine ilisema kura hiyo ilifanyika chini ya mazingira ya kulazimishwa na haiwakilishi utashi wa raia wa Donetsk, Luhansk, Zaporizhzhia na Kherson.

Wiki iliyopita, Guterres alisema “kuchukuliwa kwa eneo la nchi na nchi nyingine kwa kutumia vitisho au nguvu ni ukiukaji wa kanuni za mkataba wa Umoja wa mataifa na sheria za kimataifa.”

Huku Russia ikiendelea na mchakato wa madai ya kunyakuwa maeneo ya Ukraine, vikosi vya Ukraine vilichukua tena udhibiti wa maeneo yaliyokuwa yanashikiliwa na Russia.

XS
SM
MD
LG