Jeshi la Ujerumani lilisema vikosi vyake na vile vya kutoka Marekani walihusika katika mapambano hayo.
Uwanja wa ndege umekuwa mahali pa kuhamishwa kwa umati wa watu unaofanywa na mataifa ya magharibi, hasa tangu Taliban ilipokamata mji mkuu wa Afghanistan, wiki moja iliyopita.
Maelfu ya raia wa Afghanistan wamefurika katika uwanja wa ndege wa Kabul kwa matumaini ya kupata nafasi kwenye moja ya ndege za kuwaondoa nchini humo.
Raia hao wanahofia kurudi kwa utawala wa tafsiri kali ya sharia za Kiislam, wakati Taliban ilipodhibiti nchi hiyo miaka 20 iliyopita.
Marekani imeshindwa kuwahamisha watu 5,000 hadi 9,000 kwa siku, na matukio ya machafuko Dani na karibu na uwanja wa ndege yamesababisha kukosolewa kwa juhudi zake hizo.