Wakati huohuo biashara kwenye masoko ya Ulaya ikiwa katika hali ya mchanganyiko.
Kipimo cha hisa cha London FTSE kilikuwa chini kwa asilimia 0.4, wakati kile cha Paris CAC-40 na cha Frankfurt DAX biashara yake ilikuwa imeshuka kwa asilimia 0.2.
Masoko ya Asia yalimaliza siku mengi kati yao yakiwa juu Jumatano, wakati kipimo cha hisa cha Hong Kong Hang Seng kikipanda kwa asilimia 1.1, na kile cha Shanghai kilimaliza siku kikiwa juu kwa asilimia 0.6 katika kipindi cha kwanza cha biashara baada ya mapumziko ya muda mrefu.
Kipimo cha hisa cha Korea Kusini KOSPI kilipanda kwa asilimia 1.7, wakati kile cha Taiwan TSEC 50 haikuwa na mabadiliko yoyote na ile ya S&P/ASX ilipata hasara ya asilimia 0.4.
Na nchini Marekani biashara kwenye masoko ya fedha kwa vipimo vya Dow Jones, S&P 500 na Nasdaq ilifungwa jana jioni ikiwa imepanda kwa asilimia 0.8.
Katika biashara ya mafuta, bei ya mafuta ghafi ya kipimo cha West Texas Intermediate kilikuwa dola za Marekani 24.40 kwa pipa, ikiwa juu kwa asilimia 3.4 wakati kile cha soko la kimataifa cha Brent bei ya mafuta ghafi ilikuwa dola 31.74, kwa pipa, ikiwa imepanda kwa asilimia 24.