Marekani yatangaza kupunguza gesi chafu 2030

Mkutano kwa njia ya video juu ya mabadiliko ya hali ya hewa ulimwenguni.2021

Rais wa Marekani Joe Biden ametangaza Alhamisi lengo jipya la kupunguza uchafuzi wa gesi chafu Marekani kwa asilimia 50 hadi 52 ifikapo mwaka 2030.

Amesema dunia lazima "idhibiti janga linalo hatarisha maisha yetu katika zama zetu," wakati anaongoza mkutano kwa njia ya video juu ya mabadiliko ya hali ya hewa ulimwenguni.

Lengo la Marekani linahusu viwango vya 2005, na White House inasema juhudi za kufikia ni pamoja na kuelekea kwenye umeme bila uchafuzi wa kaboni.

Pia taifa hili litaboresha ufanisi kwenye mafuta ya magari na malori, kusaidia kukamata kaboni kwenye vituo vya viwandani na kupunguza matumizi ya Methane.

Afisa katika utawala wa Biden aliwaambia waandishi wa habari katika mkutano wa Jumatano, kwamba kwa lengo jipya la Marekani na yale yaliyowekwa na Japan, Canada, Uingereza na Jumuiya ya ulaya, kwa jumla uchumi mkubwa unaosimamia zaidi ya nusu ya uchumi wa ulimwengu, sasa utajitolea kasi ya upunguzaji wa hewa chafu iliyohitaji ulimwengu kupunguza joto hadi digree 1.5.