Marekani yaandaa vikwazo vipya dhidi ya Iran

Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Mike Pompeo akutana na Prince Mohammed bin Salman wa Saudi Arabia June 24, 2019. Jacquelyn Martin/Pool via REUTERS - RC1F09C21CC0

Marekani inatarajiwa kuiwekea Iran vikwazo vipya, Jumatatu, ikilenga kuongeza msukumo zaidi kwa uchumi wa nchi hiyo ili kubadilisha tabia ya serikali yake.

Waziri wa Mambo ya nje wa Marekani Mike Pompeo ametaja hatua hizo mpya kuwa muhimu lakini akakataa kutoa maelezo zaidi kwa waandishi wa habari kabla ya tangazo rasmi.

Pompeo alikuwa akizungumza alipowasili kutoka Saudi Arabia na Umoja wa Falme za kiarabu, alikozuru kuendeleza juhudi za utawala wa Rais Donald Trump za kujenga umoja wa washirika ili kukabiliana na Iran.

Iran imekanusha kwamba inatengeneza silaha za nuclear, na ilisaini mkataba wa mwaka 2015 na Marekani, Uingereza, China, Ufaransa, Russia na Ujerumani ili kuondoa hofu hiyo.

Imetayarishwa na mwandishi wetu, Washington, DC