Watu 51 wamekufa kufuatia mafuriko na maporomoko ya matope katika mji wa Durban, na eneo kubwa la majimbo la Kwa zulu-Natal, nchini Afrika kusini.
Sehemu za kusini na mashariki mwa Afrika kusini, zimekumbwa na mvua kubwa katika siku za hivi karibuni, huku mafuriko Zaidi na upepo mkali ukitarajiwa katika sehemu za pwani.
Tayari utabiri wa hali ya hewa unaonyesha kimbunga Kenneth chatarajiwa kupiga katika maeneo ya pwani ya kusini mashariki ya Afrika ikiwemo Tanzania, Comoros, na Msumbiji.
Nchini Afrika Kusini baadhi ya barabara zimeharibiwa huku nyumba zikiwa zimeanguka kutokana maporomoko ya matope.
Darzeni ya watu wamepelekwa hospitalini kwa matibabu huku juhudi za uokoaji zikiendelea kuwatafuta manusura chini ya vifusi vya nyumba zilizoanguka.
Imetayarishwa na mwandishi wetu, Washington, DC.