Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 22:43

Milipuko ya kipindupindu, kuharisha yaikumba Msumbiji


Watoto wa kike wakiteka maji katika kambi ya makazi ya muda ya manusura wa kimbunga Idai, Beira, Msumbiji, April, 2, 2019.
Watoto wa kike wakiteka maji katika kambi ya makazi ya muda ya manusura wa kimbunga Idai, Beira, Msumbiji, April, 2, 2019.

Shirika la afya duniani, WHO, limetangaza Jumanne kwamba watu 1,052 wameambukizwa ugonjwa wa kipindupindu na kuna watu 2,700 wenye ugonjwa wa kuharisha huko msumbiji.

Mlipuko huu umetokea wiki mbili baada ya kimbunga Idai kusababisha maafa na uharibifu katikati ya maeneo ya Msumbiji.

Mwandishi wa VOA anaetembelea mji wa Buzi anaripoti kuwa hadi sasa bado inawawia vigumu kwa vyombo vya serikali na mashirika ya misaada ya kibinadamu kufikia miji na vijiji kutokana na kuharibika kwa barabara na madaraja baada ya mafuriko makubwa.

Wakati maji ya mafuriko yanapopunguka maelfu na maelfu ya watu waliokimbia makazi yao wanarudi kushuhudia hasara walizopata wengi wakiwa wamepoteza makazi yao. Wengine wengi bado wakiwa wanawatafuta waliofariki ili kukamilisha mazishi yao.

Katika mji huu wa Buzi, mkazi Sabe Magamboa, alimzika mama yake siku ya Jumamosi lakini hivi sasa anatafuta chakula.

Sabe Magamboa, Mkazi wa Buzi anasema :"Niko pekee yangu. Sina mtu wa kumtegemea. Siwezi kufanya kazi sina nguvu ya kufanya chochote. Nina mgonjwa nyumbani. Kilichobakia hivi sasa ni kwenda kutafuta chakula, na nikipata niweza kula na familia yangu.

Hiyo basi ni hali inayowakabili maelfu ya wakati wa miji mbali mbali ya Msumbiji, Malawi na Zimbabwe baada ya kimbunga Idai kusababisha mafuriko makubwa mwezi uliyopita.

Shirika la afya dunian, WHO, linaeleza kwamba changamoto kubwa hivi sasa ni kukabiliana na magonjwa yanayosababishwa na maji machafu na msemaji wake Christian Lindneier anasema wameanza kufungua vituo vya matibabu na kampeni za machanjo.

Christian Lindmeier:" Vituo saba vya matiubabu vimefunguliwa venye jumla ya vitanda 400 hadi hivi sasa na vinachukuwa wagonjwa. Kuna dawa za chanjo laki 9 zinazotarajiwa kuwasili Jumatano. Na kampeni imepangwa kuanza mara moja."

Anasema kampeni kwa hivi sasa itafanyika katika mji wa Beira na wilaya tatu za Buzi, Dondo na Nhamatanda.

Madaktari kutoka China wameanza kunyunyuiza dawa katika wilaya mbali mbali kupambana na mbu wenye kueneza vidudu vya homa ya Malaria , huku wafanyakazi wa kimataifa wakigawanya chakula.

Rais Filipe Nyusi wa Msumbiji akitembelea maeneo yaliyoathirika anasema hivi sasa kuna kazi kubwa ya ujenzi wa miundo mbinu na kurudisha huduma muhimu za msingi.

Rais wa Msumbiji, Filipe Nyusi, amesema baada ya wiki mbili za operesheni ya kutafuta na kuokowa watu, juhudi za dharura hivi sasa zinaingia katika awamu mpya ya kutoa huduma za dharura kwa familia zinazohitaji mahitaji muhimu.

Kulingana na tume ya uchumi ya Umoja wa Mataifa kwa ajili ya Afrika kanda nzima lililokumbwa na janga hili huenda limepoteza miundombinu yenye thamani ya dola bilioni moja.

Imetayarishwa na Mwandishi wetu, Abdushakur Aboud, Washington, DC

XS
SM
MD
LG