Kremlin ina nia ya kuhalalisha tena kwa haraka utawala wa Assad ikikusudia kuwa hatua hiyo itaisidia Syria kujipatia misaada ya kujenga tena taifa hilo liloharibiwa na vita na kuendelea kuimarisha tena utawala wake.
Russia inaiangazia Misri, umoja wa falme za kiarabu (UAE), Iraq na Saudi Arabia katika harakati zake za kidiplomasia katika kuiunga mkono serikali ya Assad, ikiwa na nia ya kutengeneza njia ya Syria kurudishwa tena kwenye umoja wa mataifa ya Kiarabu wakati wa mkutano wa viongozi w nchi hiyo mwezi ujao huko Tunis.
Suala la Syria juu ya uwezekano wake wa kurejeshwa katika Umoja huo haliko hivi sasa kwenye ajenda ya mkutano huo utakaofanyika Machi 31, 2019, lakini wanadiplomasia wa Russia kwa sirisiri wamekuwa wakihimiza wanachama wenzao kuleta pendekezo hilo.
Umoja wa mataifa ya kiarabu wenye wanachama 22 uliiondoa Syria mwaka 2011 ikiwa ni hatua ya kupinga ukandamizaji wa kinyama unaofanywa na utawala huo dhidi ya watu wake hasa waislamu wa kisunni walioongoza upinzani dhidi ya Assad.
Baadhi ya matiafa yaliondoa mabalozi wao mjini Damascus. Katika siku za karibuni baadhi ya balozi zimefunguliwa tena mjini humo licha ya ushahidi kuwa wakimbizi wanaorudi nyumbani kutoka ulaya na mataifa mengine wanakamatwa au kulazimishwa kuijiunga na jeshi.