Jopo la Seneti lapokea ushahidi juu ya China kuzisaidia serikali za kidikteta kuwadhibiti raia

Seneta Bob Menendez

Wabunge nchini Marekani, na watetezi wa haki za binadamu wanaishutumu China kwa kueneza mfumo wa kiimla huku ikiziunga mkono serikali za kidikteta na zenye ukandamizaji duniani, kuwapeleleza na kuwadhibithi raia wake.

Shutuma hizo zinajiri miaka 30 baada ya ukandamizaji uliyofanywa dhidi ya waandamanaji katika eneo la uwanja wa Tiananmen Square, nchini China.

Mwenyekiti wa ngazi ya juu wa kamati ya uhusiano wa kimataifa katika baraza la seneti, Bob Menendez, amesema ni lazima Marekani ichukuwe hatua madhubuti zaidi kuhakikisha haki za binadamu zinaheshimiwa badala tu ya kuzungumzia hali hiyo.

“Inatatiza na kusikitisha kusikia tangazo la Waziri wa Mambo ya Nje Pompeo wiki iliyopita linaloeleza kuundwa kwa tume mpya kuhakikisha uwepo, nukuu na tafsiri sahihi ya haki za binadamu. Ukweli ni kuwa tafsiri imara ipo tayari. Hatuhitaji kutafsiri tena haki za binadamu, kinachotakiwa ni kutetea na kulinda haki hizo. Ni lazima tuziunganishe zana zetu na vitendea kazi vyetu. Lazima tujenge ushirikiano imara wa kidiplomasia na usalama. Lazima tuimarishe uwepo wetu., amesema Menendez.

Waliotoa ushahidi mbele ya jopo hilo wameeleza kuwa uwekezaji wa nguvu wa China katika teknolojia ya kufuatilia watu mahali walipo, katika mawasiliano na mitandao – China inawajengea uwezo huo serikali katika bara la Afrika, Asia, mpaka Amerika ya Kati.

Seneta wa Republikan James Risch amesema China inatumia fursa ya uwazi katika kuendeleza demokrasia kukandamiliza uhuru wa kujielezea.