Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Novemba 23, 2024 Local time: 13:50

Juhudi za kuipamba China zinakabiliwa na changamoto nyingi


Rais Xi Jinping
Rais Xi Jinping

Serikali ya China inatumia milioni ya dola kila mwaka katika juhudi ya kueneza mitizamo yake nje ya nchi, lakini kiwango hiki cha matumizi ya fedha kimekumbana na vipingamizi.

Hilo ni kuanzia kukataliwa kwa Taasisi za Confucius katika vyuo vikuu nje ya nchi mpaka malumbano ya vikundi vya wanafunzi katika kuzungumzia masuala ya Dalai Lama.

Katika miezi ya karibuni, “kampeni kushawishi wanaaminika” inayofanywa na Beijing nchini Marekani vimekuwa chini ya uchunguzi zaidi, hasa vitega uchumi vyao huko Hollywood.

Pia kumekuwa na wasiwasi juu ya utawala wa mabavu wa Chama cha Kikomunisti ambacho kinataka kueneza mtindo wake wa kukandamiza na kuzuia habari. Lakini wasiwasi huo, wachambuzi wanadai kuwa, umekuzwa kupita kiasi.

Kutoa habari za China

Wakati uwezo wa uchumi wa China umepanuka na ushawishi wake umekua duniani, Beijing inatafuta njia kusahihisha kile inachokichukulia kuwa ni upotoshaji wa sura yake halisi.

Rais wa China Xi Jinping mara nyingi anaongea kuhusu kile anachosema ni juhudi ya “kueleza habari za China vizuri”-kueleza habari zao kwa maelezo yao wenyewe.

Beijing inadhamiria kuitangaza China kama “ni ustaarabu wa kale, unaojitosheleza,” amesema Clayton Dube, mkurugenzi wa Chuo Kikuu cha Southern California Taasisi ya Marekani –China.

“Kutokana na kukua kwa uchumi wa China, imeweza kuwekeza kwa nguvu zote katika kukuza teknolojia za mawasiliano ya kisasa, kuwekeza kwa nguvu katika utangazaji, kuwekeza katika internet, tovuti na ukusanyaji habari na mambo kama hayo, lakini pia kuwekeza katika Taasisi za Confucius ilikuwafanya Wamarekani waielewe zaidi China.

Baadhi ya mambo haya yanafanyika kwa uwazi kupitia vyombo vya habari vya utangazaji vya serikali kama vile kituo cha kati cha Televisheni ya China, ambacho hivi karibuni kimezinduliwa upya na kuitwa China Global Television Network, or CGTN. Pia kinajitangaza katika mfumo wa “Tangazo lenye maoni” katika magazeti mengi makubwa ya Marekani.

Yako mambo mengine yaliojificha

Katika vyuo vikuu, kuna Taasisi za Confucius, zaidi ya lugha 100 za Kichina na vituo vya kujifunza ambavyo kuongezeka kwake kunaonekana katika vyuo vikuu na taasisi za masomo ya juu nchini Marekani.

Vituo hivyo vinadai kuwa sio vya kiserikali, lakini kiutawala, kikundi cha wadhamini wake wako chini ya Wizara ya Elimu ya China.

Na katika miaka ya karibuni, vituo kadhaa vimefungwa juu ya madai kuwa haviko wazi na kuna athari zilizojitokeza katika uhuru wa kielimu.

Philip Clart, Mkurugenzi wa Taasisi ya Confucius ya Chuo Kikuu cha Leipzig na Profesa wa masomo ya Kichina katika kitengo cha Tafiti za Asia ya Mashariki (East Asian Studies), anatoa hoja kuwa linapokuja suala la Taasisi za Confucius, zinaweza kuwa na faida kama zitasimamiwa ipasavyo.

Clart amesema kuwa wakati suala la udhibiti na uhuru wa maoni linabakia kuwa ni tatizo, hivi vitu sio kwamba vinashinikizwa katika program hiyo na vinaweza kuepukwa iwapo kuna kutenganisha kuliko wazi katika utendaji na matumizi yake kati ya program hiyo na chuo kikuu.

Lakini, “iwapo upo katika sehemu ambayo hakuna kitengo cha masomo ya Kichina au Asia yenye kujitegemea, ambapo Taasisi ya Confucius inapewa fursa kwa mara ya kwanza kuweza kutoa mchango wake, muongozo wowote wa Kichina, na hakuna sauti nyingine, hili linaweza kuwa jambo gumu.”

Jinsi ya kuupamba udikteta

Makundi ya wanafunzi wa Kichina pia ni nguvu inayoongezeka ambayo wakati mwengine imeonyesha kusimamia ajenda ya Chama cha Kikomunisti nchi za nje.

Kwa mfano, wakati kiongozi wa kiroho wa Tibeti ambaye yuko ukimbizini, Dalai Lamaa alipokaribishwa Chuo Kikuu cha California, San Diego Juni, kikundi cha wanafunzi wa Kichina hapo chuoni kilianzisha maandamano kumtaka asitoe hotuba yake.

Wakati kikundi hicho kilipo kusanyika kupinga mwaliko huo, kikitoa hoja ya kustaajabisha sana kwamba mwaliko wa Dalai Lama unakwenda kinyume na “kuheshimu tabaka mbalimbali” na “msimamo sahihi wa kisiasa,” na hapo ndipo mahusiano yao na ubalozi mdogo wa China ulipojitokeza hadharani.

Tukio hilo na mengine yamekuwa yakiashiria ugumu ambao Beijing inakabiliwa nao na vipi mstari kati ya kutoa habari za China na kueneza propaganda ya Chama cha Kikomunisti vinavyoweza kujichanganya.

Njia mbalimbali za vyombo vya habari

Utafiti wa shirika la habari la Reuters wa 2015 umeonyesha kuwa zaidi ya dazeni za stesheni nchini Marekani zilikuwa zinatangaza programu kutoka idhaa ya kitaifa ya China Radio International nchini Marekani.

Na wakati ikiwa kuwafikia wasikilizaji wanaozungumza Kiingereza pengine ni tatizo, wachambuzi wanaona kuwa Chama cha Kikomunisti kimepiga hatua kubwa inapukuja katika suala la vyombo vya habari vinavyotangaza kwa lugha ya Kichina.

Wakati zikiwa zinafuatiliwa katika maeneo mengi, sehemu kubwa ya matangazo yake yanadhibitiwa na Beijing au kuwa na mafungamano nayo. Kwa sehemu kubwa inalenga Watu wenye asili ya China ambao pengine wanasikiliza matangazo ya Kiingereza, lakini inazirekebisha na kwa namna fulani inaminya habari wanazopokea.

Hatimaye, lengo la Chama cha Kikomunisti ni kufanya “kikubalike kama chenye uwezo, uhalali na uzuri,” anasema Robert Daly, Mkurugenzi wa Taasisi ya Kissinger inayotafiti China na Marekani katika Kituo cha Woodrow Wilson. Lakini kuuza udikteta wa chama kimoja ni “uwanja mgumu sana.”

“Watu wanaisikiliza China, watu wanaijua China ni muhimu, lakini wao (Beijing) kwa kweli hawana habari nzuri ya kuelezea kuwaridhisha Wamarekani kuwa udikteta wa chama kimoja, kwa kweli, uko sawa,” Daly amesema.

XS
SM
MD
LG