Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 16:20

Trump, Sissi kuongeza ushirikiano dhidi ya ugaidi


Rais Abdel Fatah el-Sissi
Rais Abdel Fatah el-Sissi

Marekani na Misri zinatarajiwa kufikia makubaliano katika kuongeza ushirikiano katika vita dhidi ya magaidi wa kiislamu wenye msimamo mkali Jumatatu wakati Rais Abdel Fattah el-Sissi atakapomtembelea Rais Donald Trump huko White House.

"Viongozi hao wote wanapinga vikali siasa za kiislamu," amesema H.A Hellyer, mtafiti wa ngazi ya juu katika kituo cha Rafik Hariri kinachoshughulikia masuala ya Mashariki ya Kati katika Baraza la Atlantic.

"Wote wanaangalia masuala ya usalama kama ni kipaumbele cha kwanza, pili na tatu katika siasa."

Taarifa ya White Houseiliyotolewa mapema kabla ya ziara hiyo imesema, "Mahusiano hayo kihistoria yanapelekwa na maslahi ya kiusalama, na hilo litabakia kuwa suala muhimu katika mazungumzo yao."

Tamko hilo pia limempongeza kiongozi wa Misri juu ya sera zake kali katika kupambana na magaidi.

"Sissi amechukua hatua za kishujaa katika mambo nyeti mengi tangia alivyokuwa rais 2014," imesema.

Hiyo ni ziara ya kwanza ya kiongozi huyo wa Misri Jumatatu katika Ikulu ya Marekani.

Rais mstaafu wa Marekani, Barack Obama alisitisha misaada kwa Cairo baada ya jeshi la Misri, likiongozwa wakati huo na Jenerali Sissi, kumpindua rais wa kwanza aliyechaguliwa kidemokrasia, Mohammed Morsi 2013. Sissi alichaguliwa kuwa rais mwaka mmoja baadae.

Obama hakumkaribisha Sissi White House na alikuwa akiikosoa serikali ya kijeshi ya Misri kwa kuwakamata wafuasi wa Muslim Brotherhood, chama ambacho Morsi alikuwa akikiwakilisha kama rais. Sissi anaamini kuwa chama cha Brotherhood ni kikundi cha kigaidi.

Mkutano wa Jumatatu katika Oval Office unaangaliwa kwa makini mjini Cairo ambapo kunashauku kubwa juu ya azma ya Trump kwa Misri na ulimwengu wa kiislamu kufuatia katazo la Trump kwa raia wa nchi sita zenye Waislamu wengi kuingia Marekani.
Hata hivyo, si k mara ya kwanza viongozi hao kukutana.

Imeripotiwa kuwa viongozi hawa mazungumzo yao yalikwenda vizuri wakati mgombea Trump alipokutana na Sissi Septemba mwaka jana, pembeni, ya Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa uliofanyika huko New York.

Sissi ni kati ya viongozi watatu wa kwanza ambao watakutana na Trump wiki hii.

Siku ya Jumatano, Mfalme Abdullah wa Jordan atakuwa ni mgeni wa rais Trump.

Siku inayofuatia, Trump atasafiri kwenda kwenye jumba lake lia kifahari katika fukwe huko Mar-a-Lago, Florida kwa mazungumzo ya siku mbili pamoja na Rais wa China, Xi Jingping.

XS
SM
MD
LG