Eneo hilo la ujenzi lilioko jirani kabisa na Dubai Mall na karibu na Jengo lenye ghorofa 63 linalojulikana kama The Address Downtown Dubai Tower, ambalo liliharibiwa vibaya sana na moto wakati wa kilele cha mwaka mpya 2015.
Jengo hilo refu lijulikanalo kama Fountain Views Complex linajengwa na mwekezaji mkubwa wa Dubai, Emaar Properties ambae alijenga Mall na hoteli ambayo ilishika moto mwaka 2015. Mwekezaji huyo alikataa kutoa kauli yoyote kuhusu ajali iliyotokea leo.
Miale ya moto ilikuwa ikirindima katika jengo hilo wakati wazima moto wakirusha maji ndani. Kila dakika chache, kulikuwa na miripuko inasikika ndani ya jengo.
Vyanzo vya habari vinasema inafikiriwa kuwa miripuko hiyo inatokana na mitungi ya gesi iliyokuwa inatumiwa na wafanyakazi.
Magari ya kubeba wagonjwa yalikuwa yamesimama karibu na jengo lakini hakukuwa na dalili kuwa mfanyakazi yoyote alihitaji matibabu.
Moto ulionekan kuwa umedhibitiwa katika ghorofa za chini katika jengo hilo.
“Huduma za kupooza joto katika jengo hilo zinaendelea na magari ya kubeba wagonjwa yako tayari katika eneo hilo,” ofisi ya habari ya serikali ya Dubai imetuma ujumbe katika akaunti yao ya Twitter ukisema hakuna majeruhi walioripotiwa.