Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Desemba 25, 2024 Local time: 04:50

Mwimbaji-mtunzi Dylan wa Marekani apokea tuzo ya Nobel


Bob Dylan
Bob Dylan

Mwimbaji - mtunzi wa nyimbo, Mmarekani Bob Dylan, amekubali kupokea tuzo ya Nobel katika fasihi Jumamosi huko Stockholm, wanachama wa taasisi ya Swedish Academy na vyombo vya habari nchini humo wameripoti.

Dylan amepokea shahada ya Nobel na medali wakati wa tafrija fupi katika hoteli karibu na mahali ambako alifanya onyesho lake Jumamosi, Klas Ostergren, mwanachama wa taasisi hiyo ya Swedish Academy, ameliambia shirika la habari la "The Associated Press."

Mmoja wa wanachama wa Academy Horace Engdahl alijibu kwa kifupi “ndio” alipoulizwa na mtangazaji wa shirika la utangazaji la umma la Sweden SVT iwapo Dylan alikubali kupokea tuzo yake.

Alifanya onyesho lake baadae Jumamosi lakini hakutaja kabisa tuzo hiyo ya Nobel aliopokea. Amepanga onyesho jingine siku ya Jumapili.

‘Njia mpya ya kujielezea kiushairi”

Taasisi hiyo imemtaja Dylan “kwa kuweza kubuni njia mpya ya kujieleza kiushairi katika utamaduni adhimu wa nyimbo za Kimarekani” wakati wanamkabidhi tuzo hiyo ya Nobel ya 2016. Ni mtunzi wa nyimbo wa kwanza kupewa tuzo hiyo ya fasihi. Kabla ya hapo iliwahi kutolewa kwa watunzi wa vitabu Thomas Mann, Samuel Beckett, Gabriel Garcia Marquez na Doris Lessing.

Gwiji huyo katika utunzi, mwenye umri wa miaka 75, hakuhudhuria sherehe za kukabidhiwa tuzo ya Nobel December 10, kwa sababu ya majukumu mengine.

Katika hotuba iliosomwa kwa niaba yake wakati wa sherehe za tuzo hiyo Disemba, Dylan alieleza kushtushwa kwake kwa kuchaguliwa kwake kuwa mshindi wa Nobel.

“Iwapo mtu angeniambia huko nyuma kwamba nilikuwa naweza kuwa na nafasi ndogo ya kuwa mshindi wa tuzo ya Nobel, ningelifikiria kuwa ni fursa iliyo nadra sana kama vile kujikuta nimesimama katika mwezi,” amesema gwiji huyo.

XS
SM
MD
LG