Mtaalam wa haki za binadamu Agnes Callamard ametoa ripoti ya ukurasa 101 Jumatano akitoa ufafanuzi juu ya uchunguzi wake juu ya mauaji ya Khashoggi, mkosoaji wa serikali ya Saudi Arabia.
Khashoggi aliingia Ubalozi mdogo wa Saudi Arabia Octoba 2 na hakuonekana tena. Ushahidi ulijitokeza baadae kuonyesha kuwa aliuawa ndani ya jengo hilo la ubalozi, kukatwakatwa na mabaki ya mwili wake kuondolewa na kupelekwa mahali pasipo julikana.
Callamard alisema wakati asingeweza kujua nani aliyeamrisha mauaji hayo, serikali ya Saudi Arabia ni wazi inawajibika kwa hilo.
“Haimkiniki kuwa viongozi wa Saudia, akiwemo mtoto wa mfalme, hawakuwa na taarifa za ukiukwaji wa sheria. Ukweli ni kuwa kuna ushahidi, ushahidi wa kuaminika, unaoonyesha wamehusika na mauaji hayo.
Kile kinachotakiwa kufanyiwa uchunguzi ni kujulikana kwa kiwango gani mwana wa mfalme alikuwa anajuwa au angekuwa anajuwa kile ambacho kingempata Khashoggi na wala haijalishi iwapo alihamasisha mauaji hayo yeye moja kwa moja au kupitia mtu mwengine.
Iwapo alifanya hilo bila ya utaratibu wa sheria, au iwapo angeweza kuzuia mauaji hayo yasifanyike wakati harakati hizo zinaanza na alifeli kufanya hivyo. Haya ni jumla ya mambo ambayo naamini uchunguzi wa jinai unafaa ufanywe ukiangaza pamoja na wengine waliohusika na uhalifu huo.”
Callamard ametaja washukiwa 11 wameshtakiwa nchini Saudi Arabia kutokana na kifo cha Khashoggi, lakini kesi imefungwa na majina yawatuhumiwa hayajatolewa. Anahofia kuwa sheria haitofuata mkondo wake.
Ameeleza pia kunavizuizi kadhaa vilivyowekwa katika uchunguzi wake, uliokuwa umeanza Januari.
Khashoggi's death was condemned internationally, including by many U.S. lawmakers.
Kifo cha Khashoggi kililaaniwa kimataifa, na kati ya waliolaani ni wabunge wa Marekani.