Israeli na UAE kushirikiana kupambana na COVID-19

Bendera za Israeli (kushoto) na Umoja wa Falme za Kiarabu(UAE).

Waziri Mkuu wa Israeli Benjamin Netanyahu ametangaza Alhamisi nchi yake itashirikiana na Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) katika vita dhidi ya virusi vya ukimwi licha ya kwamba hakuna uhusiano wa kidiplomasia kati ya nchi hizo mbili. 

Netanyahu amesema ushirikiano huo utakuwa katika nyanja za utafiti, maendeleo na teknolojia, jambo ambalo anasema litaweza kuimarisha huduma za afya katika kanda zima.

Waziri mkuu huyo hakutoa maelezo zaidi lakini alisema ushirikaino huo utatangazwa rasmi na mawaziri wa afya wa nchi hizo mbili baada ya mawasiliano ya kina mnamo miezi michache iliyopita.

Tangazo lake Netanyahu linatolewa siku chache tu kabla ya Israel kutekeleza nia yake ya kukalia maeneo kadhaa ya Ukanda wa Magharibi na bonde la Jordan.

Mpango huo unaoungwa mkono na Marekani umewakasirisha sana Wapalesina na kulaaniwa vikali na jumuia ya kimataifa

Siku ya Jumatano viongozi wa Umoja wa Mataifa, Ulaya na nchi za Kiarabu. wameionya Israeli kutusu mpango huo ambar utakuwa pigo kubwa kwa amani ya Mashariki ya Kati.