Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Desemba 24, 2024 Local time: 03:42

Israel : Netanyahu atangaza ushindi wa "kishindo"


Waziri Mkuu wa Israeli Benjamin Netanyahu akihutubia katika mji wa uwanja wa ndege huko mji Lod, Israel, Disemba. 27, 2019.
Waziri Mkuu wa Israeli Benjamin Netanyahu akihutubia katika mji wa uwanja wa ndege huko mji Lod, Israel, Disemba. 27, 2019.

Waziri Mkuu wa Israeli Benjamin Netanyahu ametangaza ushindi wa "kishindo” Ijumaa, baada ya kushinda kinyang'anyiro cha kuwania uongozi wa uchaguzi wa awali na hivyo kumwezesha kuongoza chama chake cha mrengo wa kulia cha Likud katika uchaguzi mkuu utakaofanyika Machi 2020.

Waziri Mkuu wa Israel aliyetumikia kwa kipindi kirefu nafasi hiyo kuliko wengine, anakabiliwa na mashtaka ya ufisadi na uchaguzi wa tatu katika miezi 12, alipata kura asilimia 72.5 za kura zote na mpinzani wake Gideon Saar alipata kura asilimia 27.5.

Ushindi wake huo wa kiwango kikubwa umemwezesha kujizatiti katika nafasi yake ndani ya chama ambacho amekiongoza kwa miaka 20.

“Ushindi mkubwa! Asanteni wanachama wa Likud kwa kuniamini, kuniunga mkono na kunipenda,” Netanyahu ametuma ujumbe wa tweet.

“Kwa msaada wa Mungu na nyinyi, nitakiongoza chama cha Likud kupata ushindi mkubwa katika uchaguzi unaokuja na tutaendelea kuliongoza taifa la Israel kupata mafanikio yasiokuwa na mfano,” ameongeza.

Wachambuzi wengi katika vyombo vya habari walitabiri kuwa Netanyahu atashinda lakini kiwango cha ushindi huo kimepelekea vichwa vya habari kupataza sauti.

XS
SM
MD
LG