Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Desemba 24, 2024 Local time: 15:18

Uchaguzi Israel 2019 : Netanyahu ananafasi nzuri ya ushindi


Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu akiwasalimia wafuasi wake baada ya zoezi la kupiga kura kufungwa Tel Aviv, Israel, Jumatano, Aprili 10, 2019.
Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu akiwasalimia wafuasi wake baada ya zoezi la kupiga kura kufungwa Tel Aviv, Israel, Jumatano, Aprili 10, 2019.

Waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu anaelekea kuwa katika nafasi nzuri ya kupata ushindi wa muhula wa tano baada ya matokeo ya awali ya uchaguzi uliokuwa na ushindani mkubwa kuonyesha kwamba chama chake cha Likud kipo katika nafasi nzuri ya kupata ushindi na hivyo kuunda serikali ya mseto.

Huku asilimia 97 ya kura ikiwa imeshehesabiwa chama chake kilionyesha kuwa na viti sawa na chama cha mrengo wa kati cha Blue na White kinachooongozwa na mkuu wa zamani wa jeshi Benny Gantz.

Kutokana na kwamba hakuna chama chechote chenye uwezo wa kushinda chenyewe wingi wa viti katika bunge la Knesset imekuwa kawaida hivi sasa huko Israel kuwepo na majadiliano kati ya vyama ili kunda serikali ya mseto.

Likud na washirika wake wanaweza kupata kiais cha viti 65 katika bunge lenye viti 120. Pande zote zinadai ushindi katika uchaguzi huo.

Imetayarishwa na mwandishi wetu, Washington, DC.

XS
SM
MD
LG