Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Desemba 24, 2024 Local time: 16:48

Israel : Bunge lavunjwa, uchaguzi waitishwa upya


Waziri Mkuu wa Israeli Benjamin Netanyahu na Waziri wa zamani wa Ulinzi Avigdor Liberman wakiwa katika Bunge la Israeli, Knesset, Jerusalem, Mei 23, 2016.
Waziri Mkuu wa Israeli Benjamin Netanyahu na Waziri wa zamani wa Ulinzi Avigdor Liberman wakiwa katika Bunge la Israeli, Knesset, Jerusalem, Mei 23, 2016.

Bunge la Israel mapema Alhamisi limepiga kura ya kuvunja na kuitisha uchaguzi wa pili wa haraka mwaka huu baada ya Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu kushindwa kuunda serikali ya muungano.

Wabunge wamepiga kura 74 dhidi ya 45 na sasa uchaguzi mwingine utafanyika septemba 17.

Netanyahu alikuwa na siku moja tu ambayo ni Jumatano, inayompa fursa ya kuunda serikali mpya baada ya kushinda uchaguzi wa Aprili 9.

Netanyahu alitarajia kuunda serikali ya muungano ya chama chake cha kikonsavative cha Likud akishirikiana na mrengo mwingine wa kikonsavative unaongozwa na waziri wa ulinzi Avigdor Lieberman.

Hata hivyo mashauriano yalivunjika baada ya Netanyahu na chama cha Orthodox kukataa wito wa Lieberman kwamba Wayahudi wenye msimamo wa kidini waingizwe kwenye jeshi la Israel sawa na vijana wengine wa Israel.

Imetayarishwa na mwandishi wetu, Washington, DC

XS
SM
MD
LG