Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Desemba 24, 2024 Local time: 15:11

Netanyahu ameshindwa kuunda serikali ya mseto Israel


Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu akizungumza kwenye bunge la Israel linalojulikana kama Knesset, Mei 27, 2019.
Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu akizungumza kwenye bunge la Israel linalojulikana kama Knesset, Mei 27, 2019.

Ni pigo kubwa kwa Netanyahu kushindwa kuunda serikali baada ya ushindi alioupata April 9 mwaka huu na kiongozi wa upinzani wa chama cha Blue and White anasema chama chake kipo tayari kuungana na chama tawala cha Likud ikiwa kitaongozwa na kiongozi mwingine

Wapiga kura wa Israel wanalazimika kushiriki katika uchaguzi mkuu wa pili mwaka huu baada ya mwanasiasa mkongwe Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu kushindwa kuunda serikali ya mseto baada ya juhudi za wiki kadhaa. Upinzani unachukulia hiyo ni njama ya kiongozi huyo kutaka kun’gan’gania madaraka kwa kuwalazimisha wabunge wenzake kulivunja bunge ili uchaguzi mpya uitishwe.

Kufanya hivyo inamuokowa Netanyahu kulazimikia kuachia madaraka na kumruhusu Rais Reuven Rivlin kumchagua mbunge mwingine ili kujaribu kuunda serikali.

Ingawa ni pigo kubwa kwa Netanyahu kushindwa kuunda serikali baada ya ushindi alioupata April 9 mwaka huu lakini ni nafasi nzuri kwake kujaribu tena kuwashawishi wapinzani na umma katika uchaguzi unaotarajiwa kufanyika septemba 17 mwaka huu.

Sauti ya Amerika-VOA ilizungumza na mchambuzi wa masuala ya kisiasa David Monda akiwa Johanesburg huko Afrika kusini na kumuliza kwanza kwanini anadhani Netanyahu alishindwa kuunda serikali mpya.

please wait

No media source currently available

0:00 0:03:27 0:00

Netanyahu anafahamu ifikapo mwezi Julai atakua WaziriMkuu aliyetawala kwa muda mrefu Israel kumpita baba wa taifa David Ben-Gurion.

Benny Gantz, kiongozi wa upinzani wa chama cha Blue and White
Benny Gantz, kiongozi wa upinzani wa chama cha Blue and White

Kiongozi wa upinzani Benny Gantz wa chama cha Blue and White chenye msimamo wa kati anahisi ni njama ya Netanyahu kubaki madarakani lakini alisema chama cha Blue and White kipo tayari kuunda mungano na chama cha Likud ikiwa kitaongozwa na kiongozi mwingine. Hawataki kujihusisha na Netanyahu ambae anakabiliwa na mashtaka ya ulaji rushwa na utumiaji mbaya wa madaraka na kesi yake iko mahakamani.

XS
SM
MD
LG