Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Desemba 24, 2024 Local time: 15:45

Juhudi za Kuunda Serikali : Netanyahu na Gantz watupiana lawama


Benjamin Netanyahu na Benny Gantz
Benjamin Netanyahu na Benny Gantz

Waziri Mkuu wa Israeli Benjamin Netanyahu na hasimu wake Benny Gantz wametupiana lawama Jumapili baada ya juhudi zao kugonga ukuta kufikia makubaliano ya kuunda serikali ya mseto kufuatia uchaguzi uliokwama.

Mazungumzo mapya kati ya chama cha mrengo wa kulia cha Likud kinachoongozwa na Netanyahu na chama cha Blue and White kinachoongozwa na Gantz chenye mrengo wa kati yalivunjika Jumapili na pande zote mbili ziko mbali kuweza kufikia makubaliano.

Likud imesema Netanyahu atafanya “juhudi ya mwisho” kufikia makubaliano kabla ya kumfahamisha Rais Reuven Rivlin ameshindwa kuunda serikali.

Hilo litampa fursa Rivlin kuamua iwapo amtake Gantz kujaribu kufanya hivyo au alitake bunge kukubali kumpitisha mgombea wanaekubaliana naye kuwa waziri mkuu kwa idadi ya kura zisizopungua 61 kati ya wabunge 120.

Netanyahu “atafanya juhudi ya mwisho kuweza kuunda serikali katika hatua hii, kabla ya kurudisha jukumu hilo kwa rais,” Likud imesema katika tamko lake.

Imesema mazungumzo yaliyofanyika mara ya mwisho “hayaridhishi kwa kiwango kikubwa.”

Chama cha Blue and White kimekituhumu chama cha Likud kwa “ kuwatupia mafumbo kwa nia pekee ya kutafuta kuungwa mkono katika maandalizi ya kuikokota Israel kufanya uchaguzi mwengine kwa matakwa ya Netanyahu.

Uchaguzi uliofanyika mwezi huu ni wa mara ya pili mwaka 2019, baada ya Netanyahu kushindwa kuunda serikali ya mseto baada ya uchaguzi mwezi Aprili kumalizika.

Israel inasheherekea siku mbili za sikukuu ya Rosh Hashanah kuanzia Jumapili usiku na mazungumzo ya uhakika hayatarajiwi kufanyika wakati huo.

XS
SM
MD
LG