Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Novemba 23, 2024 Local time: 14:51

Netanyahu akabiliwa na changamoto mpya ya kuunda serikali ya mseto


Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu na Mkuu wa Majeshi wa zamani Benny Gantz
Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu na Mkuu wa Majeshi wa zamani Benny Gantz

Waziri Mkuu wa Israeli anahangaika kuunda serikali ya mseto hata baada ya kumshinda hasimu wake, Mkuu wa Majeshi wa zamani Benny Gantz, katika uchaguzi uliofanyika Jumatatu uchaguzi uliorudiwa mara ya tatu mwaka huu nchini humo.

Netanyahu ambaye ni Waziri Mkuu aliyeko madarakani kwa kipindi kirefu zaidi anaupungufu wa viti vitatu ambayo vinge muwezesha kuunda serikali ya mseto.

Maoni ya awali

Ukusanyaji wa maoni ya awali Jumatatu usiku ulionyesha chama cha mrengo wa kulia cha Netanyahu na kundi la kidini watapata viti 60 kati ya viti 120 katika bunge la Knesset la Israeli.

Lakini matokeo ya uchaguzi yalibadilisha picha hiyo. Uchaguzi huo unafafana kwa namna mbalimbali na ule wa miaka miwili iliyopita na mwaka huu hakuna chama kilicho na njia ya kuunda serikali ya mseto ya waliowengi.

Waziri Mkuu Netanyahu

Netanyahu alirudi tena baada ya uchaguzi uliopita, huku chama chake cha Likud kikiwa kikubwa zaidi, na Rais wa Israel Reuven Rivlin anatarajiwa kumpa fursa ya kwanza kuunda serikali.

Netanyahu amesisitiza kuwa ameshinda kwa kishindo, pamoja na kuwa anakabiliwa na mashtaka ya kujibu ya ufisadi. Kesi yake imepangwa kuanza kusikilizwa Machi 17.

Wananchi wampa kura nyingi

Amesema kuwa wananchi wa Israeli walimpa kura nyingi zaidi katika uchaguzi wa waziri mkuu kuliko mtu yeyote katika historia ya Israel na alisema – ulikuwa ushinidi mkubwa.

Netanyahu pia ametuhumu Gantz kwa kujaribu kudhoofisha matokeo ya uchaguzi huo kwa kushinikiza kuwepo sheria itakayo weka katazo kwa waziri mkuu kuendelea kutumikia wadhifa wake wakati akiwa amefunguliwa mashtaka.

Wachambuzi wanawasiwasi

Wachambuzi wanasema haitakuwa rahisi kupitisha sheria hiyo kwa haraka na haitarajiwi kumgusa waziri mkuu hivi sasa.

Mwandishi wa habari wa Israeli Amotz Asael anasema Netanyahu ameshinda, lakini anasafari ndefu ya kisiasa mbele yake.

“Huu siyo ushindi wa kishindo. Hili haliwapi fursa na nguvu za kutawala kama wanavyosema. Hili haliwafanyi wao kwa ushindi huo kuunda serikali inayotarajiwa waunde ili waweze kumaliza mvutano wa kisiasa ambao tumekuwa nao hapa nchini kwa mwaka mzima,” alisema Asael.

Netanyahu anahitaji wajumbe watatu

Netanyahu ni lazima ajaribu kupata angalau wajumbe watatu wa mrengo wa kati kubadilisha msimamo wao na kuiunga mkono serikali yake. Gayil Talshir, profesa wa sayansi ya kisiasa huko Chuo Kikuu cha Hebrew, anasema hilo siyo rahisi kutokea.

“Ukweli ni kuwa sioni hilo kutokea japokuwa wafuasi wa Likud wanafanya bidi kubwa kuwapata wale waliotayari kuhama chama chao lakini ilivyokuwa kwamba ni uchaguzi uliofungamana na itikadi, sioni kabisa uhakika wa wale watakao kuwa tayari kuhama vyama vyao, na sifikirii iwapo Likud itakaposhindwa kupata kura 61 wataweza kuwavuta makubaliano hayo kwa maslahi yao.

XS
SM
MD
LG