Akizungumza na waandishi habari Alhamis mjini Khartoum msemaji wa serikali Faisal Mohamed Salih amasema suala la uhusiano Israel sio jukuma la serikali ya mpito kulishughulia.
Salih amefafanua kuwa Mkuu wa Baraza la mpito amethibitisha kwamba alichukuwa binafsi jukumu hilo na hakushauriana na mtu yeyote na anachukua dhamana yote kuhusiana na suala hilo.
Mkutano wa siri kati ya Jenerali Burhan na Waziri Mkuu Netanyahu mjini Entebbe mapema mwezi Februari ulizusha utata mkubwa nchini Sudan, pale waziri mkuu wa Israel alipotangaza kuwa Khartoum itafunguwa ubalozi wake Israeli karibuni.
Kimsingi Israel inaendelea kuwa katika hali ya vita na Sudan ambayo iliunga mkono makundi ya Kiislamu yenye itikadi kali chini ya utawala wa Omar Al Bashir aliyepinduliwa mwaka 2019.
Jeshi la Sudan limesema linaunga mkono mazungumzo kati ya Burhan na Netanyahu kwa vile ilikuwa ni kwa maslahi ya usalama wa taifa ya nchi.
Imetayarishwa na mwandishi wetu, Washington, DC.