Ving’ora vililia wakati wa usiku katika eneo Beersheba, mji mkubwa kuliko yote upande wa kusini mwa Israel, kiasi cha kilomita 35 kutoka mpaka wa Gaza, wakionya shambulizi lililokuwa njiani.
Jeshi hilo la Israel limesema mfumo wake wa kuyazuia makombora ulizuia mashambulizi hayo mawili.
Masaa machache baadae, ndege za Israeli za kivita zilishambulia vituo kadhaa vya kivita vinavyoendeshwa na Hamas, kikundi cha Kiislam kinacho tawala Gaza. Hakuna majeruhi walioripotiwa.
Shambulizi hilo la kombora lilikuja takriban siku mbili baada ya makubaliano ya kuacha mapigano kumaliza mashambulizi yanayovuka mipaka kati ya Israel na kikundi kidogo cha wapiganaji wa Palestina, Islamic Jihad.
Mapambano mabaya kuliko miezi yote yalitokea Jumanne wakati Israel ilipomuua kamnda wa ngazi ya juu kutoka kikundi kinachosaidiwa na Iran cha Islamic Jihad, ikimuangalia kama kitisho kikubwa kwao.