Iraq, Iran zakubaliana kuimarisha ushirikiano wa biashara, uwekezaji

Rais wa Iraq Barham Salih (Kati) na mgeni wake Rais wa Iran Hassan Rouhani, wakikagua gwaride la heshima lililoandaliwa kumkaribisha kiongozi huyo huko katika kasri ya Salam, Baghdad, Iraq, Jumatatu, Machi 11, 2019.

Viongozi wa Iraq na Iran wamekutana na kufanya mazungumzo Jumatatu mjini Baghdad na kufikia makubaliano, pamoja na mambo mengine, kuimarisha ushirikiano kati ya nchi hizo mbili, katika nyanja za biashara, na uwekezaji.

Rais wa Iraq Barham Salih amesema : Tumefanya mazungumzo na Rais Hassan Rouhani juu ya umuhimu wa kujenga mahusiano mema na kuendeleza uhusiano huo katika misimamo ya kiuchumi. Pia tumekubaliana juu ya umuhimu wa kuimarisha biashara kati ya nchi hizi mbili na kuanzisha miundombinu za uchumi katika ya nchi zetu na wananchi wake.”

Shirika la Habari la AFP limesema nchi hizo zinaangaza kuimarisha ushirikiano wa pamoja katika nyanja zote, kama vile ushirikiano wa kibiashara, maeneo ya uwekezaji, kuanzisha miji ya viwanda ya pamoja, biashara ya mpakani, ushirikiano wa utalii kati ya nchi hizo mbili.

Maeneo mengine ni ziara baina ya wananchi wa Iran na Iraq, ushirikiano katika nyanja za nishati, gesi, umeme, mafuta, benki, huduma za kiufundi na uhandisi na maeneo ya barabara na reli, maji. Pia masuala mengine husika ni mazingira na masuala ya kitaifa na kimataifa..

Rais wa Iran Hassan Rouhani amewasili Baghdad Jumatatu, televisheni ya Iraqi imesema, akiwa katika ziara yake rasmi ya kwanza kwa taifa hilo ambayo Tehran iliwahi kupigana vita vilivyomwaga damu dhidi ya nchi hiyo na baadae hivi sasa inapambana na kikundi cha Islamic State.

Tangu Rouhani achaguliwe mwaka 2013, Iraq imekuwa ikitegemea askari wake wamiamvuli kupambana na IS, kufuatia mji wa Mosul wa Iraqi kutekwa na wapiganaji wa kikundi cha IS na maeneo mengine nchini Iraq na Syria.

Hivi sasa wakati wapiganaji hao wa IS wakiwa wakiwa wanaemewa kushindwa vita katika eneo la kijiji cha Baghouz, Syria, Iran inaangaza msaada wa Iraq wakati ikikabiliwa na kampeni ya Rais Donald Trump yenye msimamo mkali dhidi yake ambao hauwezi kuzuiwa baada ya uamuzi wake kuiondoa Marekani katika mkataba wa Tehran wa Nyuklia ulisainiwa na nchi zenye nguvu duniani.

Rouhani amepokelewa kwa gwaride la heshima wakati akiwasili Baghdad, ambako alikaribishwa na Waziri wa Mambo ya Nje wa Iraq Mohammed Ali Al-Hakim. Awali ya yote atazuru eneo takatifu la Mashia katika mji mkuu wa Iraq na baadae atakutana na Rais Barham Salih na Waziri Mkuu Abdel Abdul Mehdi, na pia kutembelea wanasiasa wengine na viongozi wa dhehebu la Kishia.

Rouhani, katika ziara yake hiyo ya siku tatu amefuatana na ujumbe wa ngazi ya juu wa wanasiasa na wachumi kutoka nchini Iran.

Hilo linadhihirisha ni kwa kiasi gani kuna mabadiliko tangu miaka ya 1980, wakati kiongozi wa Iraq aliyetawala kwa mabavu Saddam Hussein alipoivamia Iran, na kusababisha vita vilivyodumu kwa miaka minane ambavyo viliuwa watu milioni moja. Baada ya majeshi ya Marekani kuvamia na kumuondosha Saddam madarakani. Iran ilianzisha kampeni ya kuwasaidia wapiganaji waliokuwa wakiyahujumu majeshi ya Marekani nchini Iraq.

Tehran pia ilijenga mahusiano ya kisiasa na viongozi wa Kishia wa Iraq, ambao walikuwa wakikandamizwa na serikali ya Saddam. Kiongozi wa zamani wa Iran mwenye msimamo mkali Rais Mahmoud Ahmadinejad alikuwa rais wa kwanza wa Iran kufanya ziara Iraq mwaka 2008.