Finland yatangaza rasmi inaomba uanachama wa muungano wa NATO

Waziri Mkuu wa Finland Sanna Marin (L) na Rais wa Finland Sauli Niinistö wakitangaza rasmi inaomba uanachama wa NATO katika kasri ya Rais mjini Helsinki, May 15, 2022.

Finland imetangaza rasmi kuwa inakusudia kuomba uanachama wa muungano wa NATO.

Rais Sauli Niinisto na Waziri Mkuu Sanna Marin wametangaza uwamuzi huo Jumapili katika ikulu ya Rais mjini Helsinki.

“Hii ni siku ya kihistoria,” Niinisto alisema. “Enzi mpya zimeanza.”

Tangazo la Finland kuwa inaomba kujiunga kuwa mwanachama katika umoja huo wa ushirika wa kijeshi wa Magharibi linaonekana linatokana na uvamizi wa Russia huko Ukraine.

Sweden pia inatarajiwa kuomba kujiunga na umoja huo.

Maombi ya nchi hizo mbili za Nordic kujiunga na NATO huenda yatashughulikiwa kwa haraka.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Ujerumani Annalena Baerbock, Naibu Katibu Mkuu wa NATO Mircea Geoana na Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken wakibadilishana mawazo katika mkutano wa NATO mjini Berlin, Ujerumani May 15, 2022.

“Finland na Sweden tayari ni washirika wa karibu wa NATO, “Naibu Katibu Mkuu wa NATO Mircea Geoana alisema Jumapili mjini Berlin ambako wanachama wa NATO wanakutana kujadili kuendeleza msaada wao kwa Ukraine dhidi ya uvamizi wa Russia na kupanua wigo wa ushirika wao.

Mapema Jumapili, wanadiplomasia wa ngazi ya juu kutoka Marekani na Ukraine walikutani mjini Berlin kujadili kuhusu uvamizi wa Russia na athari ambazo zimejitokeza siyo tu kwa Ukraine lakini kwa dunia nzima.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken amemhakikishia Waziri wa Mambo ya Nje wa Ukraine Dmytro Kuleba juu ya msaada wa washirika wao kwa Ukraine na kujadili miku tano ya wiki hii na kundi la G7 na mawaziri wa mambo ya nje wa NATO.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Ukraine Dmytro Kuleba na Waziri wa Mambo ya Nje w Marekani Antony Blinken wakutana Berlin.

Majeshi ya Ukraine yalianza kujibu mashambulizi Jumamosi karibu na mji unaodhibitiwa na Russia wa Izium huko kaskazini mashariki mwa Ukraine, gavana na eneo hilo alisema. Ukraine inataka kuwasukuma Russia kutoka sehemu walioko hivi sasa na kuwazuia kuwazingira maelfu ya wanajeshi wa Ukraine upande wa mashariki katika mji wa Donbas.

Russia iligeukia kuiangazia Donbas baada ya kushindwa kuuteka mji mkuu wa Ukraine, Kyiv, mara vita vilipoanza. Lakini Ukraine imechukua baadhi ya maeneo hayo, ikiwemo mji wa pili kwa ukubwa upande wa kaskazini mashariki, Kharkiv.

Ukraine”inaonekana imeshinda mapambano ya Kharkiv,” Taasisi ya Utafiti wa Masuala ya Vita, yenye makao yake Washington, imesema.

“Majeshi ya Ukraine yameyazuia majeshi ya
Russia kuyazunguka, achilia mbali kuiteka Kharkiv, na baadae kufanikiwa kuyafukuza kutoka katika maeneo ya jiji hilo, kama walivyofanya kwa majeshi ya Russia yaliyokuwa yanajaribu kuiteka Kyiv.