Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Desemba 26, 2024 Local time: 15:49

Finland kujiunga na NATO


Katibu mkuu wa NATO Jens Stoltenberg
Katibu mkuu wa NATO Jens Stoltenberg

Kiongozi wa NATO Jens Stoltenberg Alhamisi amekaribisha uamuzi wa viongozi wa Finland wa kuunga mkono hatua yakuinjinga na muungano huo.

Stoltenberg pia amesema kwamba anaamini mchakato huo utafanyika kwa urahisi na haraka iwezekanayo.Rais wa Finland Sauli Niinisto pamoja na waziri wake mkuu Sanna Marin wameeleza nia yao ya kuijiunga na NATO, hatua ambayo huenda ikabadili sera kuhusiana na namna taifa hilo litakavyo shughulikia uvamizi wa Russia nchini Ukraine.

Kwenye taarifa ya pamoja, viongozi hao wamesema kwamba kujiunga na NATO kuitaimarisha usalama wa muungano huo pamoja na usalama wake kama taifa. Wamesema kwamba ni lazima Finland iitishe uanachama wake wa NATO bila kuchelewa na kwamba wanatumai kwamba hatua za kitaifa zinazohitaji kuchukuliwa zitafanyika katika siku chache zijazo.

Viongozi hao wamesema kwamba walifikia uamuzi huo baada ya kutoa nafasi kwa bunge kujadilia pamoja na kusikiliza maoni ya umma, ikiwemo kushauriana na jirani yao Sweden. Maafisa wa Sweden wanatarajiwa kutoa tamko lao kuhusu kujiunga na NATO katika siku kadhaa zijazo. Stoltenberg amesema kwamba uamuzi wa Finland ni wa kizalendo na wenye kuheshima na NATO.

XS
SM
MD
LG