Katibu mkuu wa umoja wa mataifa Antonio Guteres ametembelea miji kadhaa iliyo nje ya mji mkuu wa Kyiv, ambapo ushahidi wa mauaji ya watu kadhaa ulipatikana baada ya wanajeshi wa Russia kuondoka sehemu hiyo.
Mapigano yameongezeka ghafla baada ya Russia kusitisha usafirishaji wa mafuta yake hadi Poland na Bulgaria, ambazo ni wanachama wa NATO, katika hatua inayoonekana kama ya kuziadhibu nchi hizo kutokana na kuunga mkono Ukraine.
Mapigano makali yanatarajiwa katika eneo la mashariki lenye viwanda, la Donbas.
Mkuu wa jeshi la Ukraine amesema kwamba wanajeshi wa Russia wameongeza mashambulizi katika sehemu kadhaa huku wakianza awamu ya pili ya uvamizi wao.
Mashambulizi makubwa yametokea nje ya Donbas.