Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Desemba 27, 2024 Local time: 02:47

Washirika wa Marekani na NATO wanaweka shinikizo dhidi ya Russia


Rais wa Marekani Joe Biden
Rais wa Marekani Joe Biden

Rais Joe Biden alisema Jumanne kwamba washirika wa Marekani na NATO wanaweka shinikizo kubwa dhidi ya Moscow siku hiyo hiyo ambayo maafisa wa Russia walitangaza mashambulizi mapya huko mashariki mwa Ukraine.

“Ninajua waandishi wa habari wananiuliza kila mara, kwa nia njema, kwa nini siku zote niko kwenye simu na viongozi wengine wa ulimwengu kujaribu kuwaweka kwenye mpangilio, Biden alisema siku ya Jumanne huko New Hampshire kuhusu simu yake ya asubuhi na viongozi wa Uingereza, Canada, tume ya ulaya, Ufaransa, Ujerumani, Italy, Japan, NATO, Poland na Romania”.

Moja ya mambo niliyofanya ni kupata nchi nyingine nyingi kukubali hii leo kuachia petrol kutoka kwenye hifadhi zao za kimkakati.

Wakati huo huo msemaji wa White House, Jen Psaki alisema kwamba Biden na viongozi hao walizungumza kuhusu kutoa zaidi misaada zaidi ya silaha na usalama kwa Kyiv.

XS
SM
MD
LG