lavrov ameongezea kwamba anaona kama muungano wa NATO unajihusisha katika vita dhidi ya Russia kwa kuipatia Ukraine silaha
Lavrov alisema hayo katika mahojiano na televisheni ya serikali ya Russia.
Amesema kwamba msingi wa makubaliano yoyote kwa ajili ya kumaliza vita nchini Ukraine utazingatia na hali ya kijeshi itakavyokuwa nchini Ukraine.
Waziri huyo wa mambo ya nje wa Russia amesema kwamba Russia inajaribu kwa kila njia kuhakikisha kwamba silaha za nuclear hazitumiki kabisa katika vita hivyo.
Uvamizi wa Russia dhidi ya Ukraine ndio mkubwa zaidi kuwahi kutoka Ulaya tangu mwaka 1945, ambapo maelfu ya watu waliuawa, kujeruhiwa, miji kuharibiwa vibaya na zaidi ya watu milioni 5 kuhamia nchi zingine.
Moscow imesema kwamba hatua yake ni oparesheni maalum yenye lengo la kuipokonya Ukraine silaha na kuilinda. Ukriane na mataifa ya magharibi yametaja uvamizi huo kuwa uchokozi dhidi ya nchi huru.