Putin amesema kwamba Russia ilikuwa ikijibu vitisho kutoka kwa mataifa hayo karibu na mpaka wao. Akihutubia wanajeshi wakati wa maadhimisho ya kushindwa na wanazi wa Ujerumani kwenye vita vya pili vya dunia, Putin alizungumzia mada ya Russia kwa dhamana ya ulinzi, ambapo Russia ilitoa miezi kadhaa kabla ya uvamizi wake kwa Ukraine hapo Februari 24, akirejea kusema kwamba kamwe hakuwa na mipango ya kumvamia jirani yake.
Kabla ya uvamizi huo, maafisa wa Marekani pamoja na NATO walikutana mara kadhaa na wale wa Russia, lakini baadhi ya madai ya Russia yalikataliwa kama vile kuahidi kuwa Ukraine kamwe haitojiunga na NATO. Putin ameongeza kusema kwamba mataifa wanachama wa NATO hawakutaka kutusikiliza na kwamba walikuwa na mipango taofauti kabisa.
Mshauri wa rais wa Ukraine Mykhailo Podolyak kwa upande wake amesema kwamba Russia haikuwa na sababu yoyote ya msingi yakulivamia taifa lake, akiongeza kwamba mataifa wanachama wa NATO hayakuwa na mpango wa kuishambulia Russia kamwe.
Mtayarishaji: Harrison Kamau