Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Desemba 26, 2024 Local time: 12:58

Marekani yapeleka msaada mpya wa silaha zenye thamani ya dola milioni 150 Ukraine


Ndege aina ya A C-17 ya mizigo imesheheni makombora na silaha, ikiwa tayari kuondoka kwenda Ukraine, April 29, 2022, katika uwanja wa ndege wa kituo cha jeshi la anga cha Dover Delaware. (Picha na AP).
Ndege aina ya A C-17 ya mizigo imesheheni makombora na silaha, ikiwa tayari kuondoka kwenda Ukraine, April 29, 2022, katika uwanja wa ndege wa kituo cha jeshi la anga cha Dover Delaware. (Picha na AP).

Rais Joe Biden ametangaza Ijumaa msaada mpya wa silaha kutoka Marekani wenye thamani ya dola milioni 150 kwa ajili ya Ukraine ili kuzima uvamizi wa Russia.

“Nina tangaza msaada mwingine wa usalama ambao utajumuisha silaha zaidi za makombora, rada na vifaa vingine kwa Ukraine,” Biden alisema, wakati akionya kuwa ufadhili unakaribia kumalizika na kulisihi Bunge la Marekani kuidhinisha fedha zaidi.

Kulingana na afisa wa ngazi ya juu wa Marekani, shehena hiyo inajumuisha silaha za makombora 155mm kiasi cha 25,000, rada ambazo zitatumika kugundua chanzo cha mashambulizi ya adui yanapotokea, vifaa vya kudhibiti mawasiliano ya kielektroniki na vipuli.

Silaha za makombora zinaelekea kutolewa kwa ajili ya makombora yaliyopelekwa hivi karibuni na Marekani aina ya howitzers.

Shehena hiyo mpya ya Ijumaa inafanya jumla ya thamani ya silaha za Marekani zilizotumwa na utawala wa Biden kwenda Ukraine – ikiwemo makombora mazito, makombora ya kutungua ndege za kivita na droni – kufikia dola bilioni 3.8 tangu Russia ilipoanzisha uvamizi wake Februari 24, Waziri wa Mambo ya Nje Antony Blinken alisema.

Shehena ya Ijumaa inaonyesha kuwa dola milioni 250 zilizokuwa zimebakia kutokana na ufadhili ulioidhinishwa siku za nyuma kwa ajili ya Ukraine zitakuwa zimemalizika kabisa. Biden alilishinikiza Bunge la Marekani kuidhinisha kiwango kikubwa cha dola bilioni 33 kwa ajili ya msaada wa Ukraine, ambao utajumuisha dola bilioni 20 za msaada wa kijeshi, na zitawea kudumu kwa miezi mitano.

kutoka (Kushoto) Waziri Mkuu wa Japan, Waziri Mkuu wa Canada, Rais wa Marekani, Chansela wa Ujerumani, Waziri Mkuu wa Uingereza, Rais wa Ufaransa, Waziri Mkuu wa Italia wakiwa katika picha ya pamoja ya viongozi wa G7 wakati wa mkutano wa NATO, Brussels, March 24, 2022. (Henry Nicholls/Pool via AP)
kutoka (Kushoto) Waziri Mkuu wa Japan, Waziri Mkuu wa Canada, Rais wa Marekani, Chansela wa Ujerumani, Waziri Mkuu wa Uingereza, Rais wa Ufaransa, Waziri Mkuu wa Italia wakiwa katika picha ya pamoja ya viongozi wa G7 wakati wa mkutano wa NATO, Brussels, March 24, 2022. (Henry Nicholls/Pool via AP)

Biden na viongozi wengine wa G-7, pamoja na Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy, wanakutana kwa njia ya mtandao Jumapili kujadili msaada wa nchi za Magharibi kwa ajili ya nchi hiyo katika mapambano dhidi ya uvamizi wa Rais Vladimir Putin.

“Marekani imetoa kiwango cha kihistoria cha msaada wa usalama kwa Ukraine kwa kasi ya haraka. Tunapeleka silaha na vifaa ambavyo viliidhinishwa na Bunge moja kwa moja katika mstari wa mbele wa ukombozi nchini Ukraine,” Biden alisema katika taarifa yake.

Hata hivyo, Biden alisema fedha za ufadhili hivi sasa zilikuwa ”zimekaribia kumalizika” na kwamba “ili Ukraine ifanikiwe,” Marekani na washirika wake lazima “waendelee kupeleka silaha na risasi Ukraine, bila ya kusitisha hatua hiyo.”

“Bunge lazima kwa haraka litowe fedha zinazoombwa kuiimarisha Ukraine katika uwanja wa vita na katika meza ya mashauriano,” alisema Biden.

XS
SM
MD
LG