Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Desemba 27, 2024 Local time: 02:29

Ukraine: Zaidi ya raia 100 wahamishwa kutoka mji wa Mariupol ulioharibiwa vibaya na jeshi la Russia


Raia waliohamishwa kutoka mji wa Mariupol wawasili kwenye kituo cha malazi cha muda katika mji wa Bizimenne, May 1, 2022. Picha ya Reuters.
Raia waliohamishwa kutoka mji wa Mariupol wawasili kwenye kituo cha malazi cha muda katika mji wa Bizimenne, May 1, 2022. Picha ya Reuters.

Raia 100 wa Ukraine Jumapili wamehamishwa kutoka kiwanda cha chuma cha Azovstal kilichoharibiwa na mashambulizi ya Russia katika mji wa Mariupol, Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky amesema.

Mji huo wa kimkakati wa bandari kwenye bahari ya Azov umeharibiwa vibaya na mashambulizi ya mabomu ya jeshi la Russia kwa mwezi wa tatu sasa, na kupelekea kiongozi wa kanisa katoliki duniani Papa Francis kuikosoa Moscow, akiwambia maelfu ya watu katika uwanja wa mtakatifu Petro Jumapili, kwamba “mji huo ulipigwa mabomu kikatili.”

“Kwa mara ya kwanza, tumepata sitisho la mapigano la siku mbili kwenye eneo hilo, na tumefanikiwa kuwaondoa zaidi ya raia 100, wanawake na watoto,” Zelensky amesema katika hotuba ya usiku kwa njia ya video.

Kundi la kwanza la watu waliondolewa kwenye kiwanda hicho wanawasili leo Jumatatu asubuhi katika mji wa Zaporizhzhia unaodhibitiwa na Ukraine, Zelensky amesema, akiongeza kuwa anatumai hali hiyo itaendelea kuruhusu watu zaidi kuhamishwa kutoka kwenye kiwanda hicho.

Huku mapigano yakipamba moto kusini na mashariki mwa Ukraine, Spika wa bunge la Marekani Nancy Pelosi, ameahidi kwamba Marekani itaendelea kuisadia Ukraine, amesema hayo akikutana na Rais Zelensky mjini Kyiv katika ziara ya kushtukiza.

Rais Joe Biden Alhamisi aliliomba bunge kuidhinisha msaada wa ziada wa dola bilioni 33 kwa Ukraine.

XS
SM
MD
LG