Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Novemba 24, 2024 Local time: 03:52

Marekani yaikosoa Russia kwa vitendo vya uhalifu wa kivita


 Jengo lililoharibiwa katika shambulizi la angani lililofanywa na Russia wakati wa ziara ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Gutteres, Kyiv April 29, 2022. Picha na AFP.
Jengo lililoharibiwa katika shambulizi la angani lililofanywa na Russia wakati wa ziara ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Gutteres, Kyiv April 29, 2022. Picha na AFP.

Wizara ya Ulinzi Ijumaa imekosoa vikali tabia ya wanajeshi wa Russia nchini Ukraine. “Ni dhahiri wanajeshi wa Russia wametenda uhalifu wa kivita,” msemaji wa Wizara ya Ulinzi John Kirby aliwaambia waandishi wa habari katika mkutano wake wa kila siku.

“Hakuna shaka juu ya hilo. Akielezea upigaji mabomu kwenye mahospitali na “wanawake wajawazito kuuwawa,” ameuita huo “ukatili usiokuwa na mfano na unyama uliovukwa mipaka ya unyama usiokuwa na mfano.

Pia msemaji huyo amegusia jinsi gani Marekani ilikuwa haijakadiria ipasavyo ukatili wa Rais Vladimir Putin kwa wananchi wa Ukraine.

Kirby Pentagon
Kirby Pentagon

“Bila shaka tunalishughulikia hili kwa dhana ya kuwa Bwana Putin alikuwa na uwezo wa kufanya kile alichokuwa anaamini ni kwa maslahi binafsi ya Russia kuwa ni kwa kutumia silaha na dhamira ya kikatili,” alisema Kirby.

“Sidhani kama tulikadiria kikamilifu kwa kiwango gani angeweza kutekeleza aina hiyo ya uovu na ukatili – na, kama nilivyosema, unyama uliopindukia – kwa watu wasiokuwa na hatia, wasiokuwa wanajeshi, ni raia, bila ya kujali nani alikuwa anawaua.”

Russia imekanusha kuwalenga raia wakati wa mashambulizi yake ya kivita huko Ukraine.

Kirby pia amekosoa busara iliyotolewa na rais wa Russia juu ya uvamizi wake.

“Na tuseme namna ilivyo, ushenzi wake, kuwa hili ni dhidi ya unazi na kuhusu kuwalinda Warussia nchini Ukraine … wakati hakuna hata mmoja wao, hakuna yeyote aliyetishiwa na Ukraine.”

Vifo nchini Ukraine

Wakati huo huo, Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani imeelezea majonzi juu ya kifo cha raia wa Marekani aliyeuawa wakati akipigana katika majeshi ya Ukraine wakati Russia ikianzisha mashambulizi mapya huko mashariki ya Ukraine.

Mwanajeshi wa zamani wa Jeshi la Majini la Marekani Willy Joseph Cancel, 22, alikuwa akifanya kazi kwa mkataba katika kampuni binafsi ya kijeshi alipouawa Jumatatu, na ni Mmarekani wa kwanza kufahamika ameuawa wakati akipigana huko Ukraine.

“Tunafahamu taarifa hizi na bila shaka tuko tayari kuwapa msaada wa kibalozi unaowezekana familia yake,” naibu msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje Jalina Porter amesema katika mkutano wa kila siku Ijumaa. “Hata hivyo, kwa kuheshimu familia yake wakati huu mgumu wa kilio, hatuna kitu cha ziada cha kutangaza.”

Vira Hyrych
Vira Hyrych

Porter pia ametuma rambirambi kufuatia kifo cha Vira Hyrych, mwandishi wa Radio Free Europe/ Radio Liberty, mtandao shirikishi wa VOA.

XS
SM
MD
LG