Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Desemba 26, 2024 Local time: 18:54

Marekani yaahidi kufungua ubalozi wake Mjini Kyiv


Mawaziri wa Marekani Lloyd Austin na Antony Blinken wamekutana na Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy mjini Kyiv, Ukraine.
Mawaziri wa Marekani Lloyd Austin na Antony Blinken wamekutana na Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy mjini Kyiv, Ukraine.

Marekani imeahidi leo kufungua  tena ubalozi wake mjini  Kyiv hivi karibuni, wakati Waziri wa Ulinzi Lloyd Austin na Waziri wa Mambo ya Nje Antony Blinken walipoutembelea mji mkuu wa Ukraine na kupongeza mafanikio hadi sasa,  baada ya Russia kuivamia nchi hiyo.

Viongozi hao wawili wamesema kwa vile waliweza kufika Kyiv ni uthibitisho wa ushupavu wa Ukraine katika kuilazimisha Moscow kuachana na shambulio katika mji mkuu mwezi uliopita na kuahidi misaada zaidi kuwazuiya wanajeshi wa Russia ambao sasa wanajaribu kusonga mbele upande wa mashariki.

Waziri Blinken alisema: “ kama ishara zaidi ya nia ya dhati, nina mpango wa kutangaza kurejea kwa wanadiplomasia wetu Ukraine, nadhani pengine tutaanzia Lviv na baadae tutahamia Kyiv, inaweza kuchukua wiki kadhaa, lakini nitatangaza kesho. Kwa kuongezea, rais atatangaza nia ya kumteuwa Bridget Brink kama balozi wetu ajaye huko Ukraine. asante sana kwa mkataba uliompa.”

Bridget A. Brink.
Bridget A. Brink.

Marekani inatoa misaada mipya wa kijeshi huko Ukraine na kurejesha msukumo mpya wa kidiplomasiua katika taifa hilo liloharibiwa na vita wakati waziri wa mambo ya nje na mkuu wa jeshi wa rais Joe Biden wanakamilisha ziara ya siri huko Kyiv.

Blinken na Austin wamemueleza rais wa Ukraine kuhusu ufadhili mwingine wa kijeshi wa kigeni na uuzaji wa silaha wa dola milioni 165.

Ilikuwa ni ziara ya ngazi ya juu ya Marekani katika mji huo tangu Russia ilipoivamia Ukraine mwezi February mwaka 2022.

Waziri wa Ulinzi Austin ameeleza : “ Hivi karibuni kama ulivyoeleza, ahadi ya misaada ya ziada ya usalama yenye thamani ya dola bilioni moja juu ya mambo mengine mengi ambayo tayari tumefanya. Rais, unaweza kujua nikiondoka hapa, nina kusudia kukusanya mawaziri kadhaa wa ulinzi na wakuu wa ulinzi ,wote wanaounga mkono , tutajadiliana kwa kuzingatia mazungumzo yetu hapa ni nini zaidi tunaloweza kufanya ili kuongeza uwezo. . Lazima ujue, watu wa Ukraine lazima wajue , kwamba tutaendelea kufanya kila tuwezalo kuhakikisha mafanikio.”

Austin na Blinken walitangaza jumla ya dola milioni 713 za misaada ya kigeni kwa ajili ya Ukraine na washirika 15 na nchi nyingine.

Wakati huo huo Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy alieleza: “ Leo hapa Kyiv, katika wakati muhimu kwa taifa letu ninashukuru sana kwamba Marekani inaisaidia sana Ukraine. ningependa pia kumshukuru rais Joe Biden binafsi kwa msaada binafsi kwa Ukraine.”

Wakati huohuo Kuendelea kwa mashambulizi ya Russia kunakuja wakati Wakristo wa Orthodox jana Jumapili walikuwa wakisherehekea sikukuu ya Pasaka.

XS
SM
MD
LG