Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Desemba 27, 2024 Local time: 08:55

Russia yafanya mashambulizi ya anga katika kiwanda cha chuma Mariupol


Watoto walioko katika hifadhi, wakati Russia ikiendeleza uvamizi Ukraine, iliyoko chini ya ardhi ikielezwa na kikosi cha Azov cha Jeshi la Ukraine, iko ndani ya kiwanda cha chuma cha Azovstal huko Mariupol, Ukraine.April 23, 2022. Azov Battalion/Handout via REUTERS .
Watoto walioko katika hifadhi, wakati Russia ikiendeleza uvamizi Ukraine, iliyoko chini ya ardhi ikielezwa na kikosi cha Azov cha Jeshi la Ukraine, iko ndani ya kiwanda cha chuma cha Azovstal huko Mariupol, Ukraine.April 23, 2022. Azov Battalion/Handout via REUTERS .

Maafisa wa Ukraine Jumapili wamesema Russia imeanzisha mashambulizi katika kiwanda cha Chuma cha Azovstal katika mji wa bandari wa kusini wa Mariupol uliozingirwa.

Wiki iliyopita Rais wa Russia Vladimir Putin aliamuru eneo la kiwanda lidhibitiwe vikali ambako majeshi ya Russia yamejaribu kulichukua kutoka mikononi mwa pengine maelfu ya wapiganaji wa Ukraine na raia ambao wameendelea kukidhibiti kiwanda hicho.

Wakati huo huo, Kamati ya Kimataifa ya Msalaba Mwekundu ilisema katika taarifa yake Jumapili kuwa “imeshtushwa sana na hali iliyopo Mariupol, ambako watu wake wanahitaji misaada ya dharura.”

ICRC imesema, “kunahitajika mara moja na bila kipingamizi njia ya kibinadamu kuruhusu maelfu ya raia kwa hiari yao kupita kwa salama na wale waliojeruhiwa kuweza kuondoka mjini humo, ikiwemo eneo la kiwanda cha Azovstal.”

Kiwanda cha chuma cha Azovstal kikiwa kimeshambuliwa kwa makombora ya majeshi ya Russia katika eneo la kuegesha meli. (Photo by Handout / Mariupol City Council / AFP) .
Kiwanda cha chuma cha Azovstal kikiwa kimeshambuliwa kwa makombora ya majeshi ya Russia katika eneo la kuegesha meli. (Photo by Handout / Mariupol City Council / AFP) .

Shambulizi la bomu katika kiwanda limekuja wakati Ukraine inaadhimisha sikukuu ya Orthodox Easter Jumapili na wakati Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy amepangiwa kukutana na Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken na Waziri wa Ulinzi Lloyd Austin huko Kyiv, mji mkuu wa Ukraine.

Zelenskyy alisema Ukraine “inatarajia vitu na silaha mahsusi,” ikiwa ni matokeo ya ziara ya kwanza ya maafisa wa serikali ya Marekani tangu Russia ilipoivamia Ukraine Februari 24.
Hakuna uthibitisho wowote wa ziara hiyo ya maafisa wa Marekani.

Siku ya Alhamisi, Zelenskyy atakutana na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres. Kabla ya mkutano wa mkuu huyo wa UN na Zelenskyy, Katibu mkuu huyo amepangiwa kukutana na Rais wa Uturuki Tayyip Erdogan huko Ankara Jumatatu na Rais wa Russia Vladimir Putin mjini Moscow Jumanne.

Maafisa wa Uingereza walisema Jumamosi kuwa majeshi ya Russia hayajakamata maeneo muhimu mapya licha ya kutangaza kuanzisha upya mashambulizi katika upande wa mashariki, wakati Ukraine imetangaza amri ya kutotoka usiku nchi nzima kabla ya Sikukuu ya Orthodox Easter Jumapili

Ukraine imesema majeshi ya Russia yamezuia juhudi za kuwaondoa raia katika eneo lililozingirwa la mji wa bandari wa Mariupol.

Baadhi ya taarifa ya habari hii imetokana na vyanzo vya habari vya AP, Reuters and AFP

XS
SM
MD
LG