Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Desemba 26, 2024 Local time: 18:38

Familia za mabaharia wa manuari ya Russia iliyopigwa na kombora wanasubiri majibu


 Moja ya manuari kuu za Russia Moskva cruiser iliyoripotiwa kupigwa na makombora yaliyorushwa na majeshi ya Ukraine.
Moja ya manuari kuu za Russia Moskva cruiser iliyoripotiwa kupigwa na makombora yaliyorushwa na majeshi ya Ukraine.

Ililichukua  jeshi la Russia zaidi ya wiki kukiri kuwa mwanajeshi mmoja alifariki na wengine 27 hawajulikani waliko baada ya moja ya manuari zake kuu  kuzama katika bahari ya Black Sea, ikiripotiwa ni matokeo ya shambulizi la kombora la Ukraine.

Kukiri huko kulitokea baada ya familia kuanza kutafuta kwa hali ya kukata tamaa watoto wao ambao, walisema, walikuwa wanahudumu katika meli hiyo na hawakurejea nyumbani, na ndugu kuuliza maswali kuhusu taarifa za awali za Russia kuwa mabaharia wote walikuwa wameodolewa.

Waziri wa Ulinzi ya Russia alisema Ijumaa katika tangazo fupi kuwa mmoja wa mabaharia alifariki na wengine 27 walikuwa hawajulikani waliko baada ya moto kuteketeza meli hiyo ya Moskva wiki iliyopita, wakati wengine 396 walikuwa wameokolewa.

Wizara hiyo ilikuwa haikutoa maelezo yoyote juu ya madai yake ya awali kuwa wanajeshi wote walikuwa wametoka kabla ya meli hiyo kuzama.

Hasara kutokana na kuzama kwa Moskva, moja ya manuari tatu za aina yake zenye kubeba makombora ya aina yake katika jumla ya manuari za Russia, ilikuwa imegubikwa na maajabu tangu wakati iliporipotiwa mara ya kwanza Aprili 14. Ukraine ilisema ilipiga meli hiyo kwa makombora.

Wizara ya Ulinzi ya Russia haikukiri kuhusu shambulizi hilo, ikisema tu kuwa moto ulizuka katika meli hiyo baada ya silaha kulipuka, na kusababisha uharibifu mkubwa.

Moscow iliendelea kusisitiza kuwa meli hiyo ilikuwa bado inaelea na inavutwa kuelekea bandarini, na saa kadhaa baadae ilikiri kuwa ilizama – katika dharuba. Hakuna picha za meli hiyo, au operesheni za uokoaji uliofanywa, zilitolewa kwa umma.

XS
SM
MD
LG