Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Desemba 26, 2024 Local time: 17:59

Zelenskyy asema anatarajia maafisa wa Marekani kutembelea Kyiv


Waziri wa Mambo ya Nje Antony Blinken na Waziri wa Ulinzi Lloyd Austin.
Waziri wa Mambo ya Nje Antony Blinken na Waziri wa Ulinzi Lloyd Austin.

Waziri wa Mambo ya Nje Antony Blinken na Waziri wa Ulinzi Lloyd Austin wataitembelea Kyiv Jumapili, Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy amesema.

“Kesho, maafisa wa Marekani wanakuja kututembelea. Nitakutana na waziri wa ulinzi [Lloyd Austin] na Antony Blinken, “Zelenskyy aliwaambia waandishi wa habari Jumamosi, katika kile kitakacho kuwa ni ziara rasmi ya kwanza ya maafisa wa Marekani tangu Russia ilipoivamia Ukraine Februari 24.

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ameiambia VOA kupitia barua pepe Jumamosi: “Hatutaki kutoa maoni.” Wizara ya Ulinzi ya Marekani haikuweza kuthibitisha taarifa hizo kwa VOA. White House pia ilikataa kusema lolote.

Maafisa wa Uingereza walisema Jumamosi kuwa wanajeshi wa Russia wameshindwa kukamata eneo jipya licha ya kutangaza kufanya mashambulizi mapya tena upande wa mashariki, wakati Ukraine imetangaza amri ya kutotoka nchi nzima kabla ya sikukuu ya Orthodox Easter Jumapili.

Ukraine imesema vikosi vya Russia vimezuia jaribio la kuwaondoa raia kutoka mji wa bandari uliozingirwa wa Mariupol.

“Operesheni ya kuwaondoa ilizuiliwa,” afisa wa mji wa Mariupol Petro Andryushchenko alisema kupitia ujumbe wa Telegram, akiongeza kuwa kiasi cha watu 200 wamekusanyika katika eneo lililowekwa na serikali kwa ajili ya kuwaondoa, lakini majeshi ya Russia “yaliwatawanya” raia hao.

Kiwanda cha chuma cha Azovstal kikiwa kimeshambuliwa kwa makombora ya majeshi ya Russia katika eneo la kuegesha meli. (Photo by Handout / Mariupol City Council / AFP)
Kiwanda cha chuma cha Azovstal kikiwa kimeshambuliwa kwa makombora ya majeshi ya Russia katika eneo la kuegesha meli. (Photo by Handout / Mariupol City Council / AFP)

Wakazi wengine waliambiwa wapande mabasi yaliyokuwa yanaelekea eneo linalodhibitiwa na Russia la Dukuchayevsk, ambalo liko kilomita 80 kuelekea kaskazini, Andryushchenko alisema.

Majeshi ya Russia yamejaribu kukivamia kiwanda cha chuma kilichopo Mariupol, eneo la mwisho lenye upinzani katika mji wa bandari uliozingirwa ambalo lina umuhimu mkubwa kimkakati, huenda likawanyima waukraine bandari muhimu, wakati ikiipa Russia njia ya ardhini kwa Crimea, ambayo Moscow iliikamata kutoka Ukraine mwaka 2014.

Russia ilifyatua makombora sita katika mji wa bandari wa Odessa huko Black Sea siku ya Jumamosi, na kuuwa watu watano, maafisa wa Ukraine wamesema. Wizara ya Ulinzi ya Russia imesema wanajeshi wake wamefanya amshambulizi ya makombora katika ghala zenye silaha huko Odesa zilizokuwa zimepelekwa kwa wanajeshi wa Ukraine zikitokea Marekani na nchi za Ulaya.

Maafisa wa Ukraine walisema Jumamosi kuwa wanajeshi wa Russia 21,600 wamefariki nchini Ukraine. Rais wa Ukraine Zelenskyy alirejea tena wito wake wakutaka kukutana na kiongozi wa Russia Vladimir Putin “kumaliza vita hivyo.”

“Nadhani yeyote aliyeanzisha vita hivi ataweza kuvimaliza,” Zelenskyy alisema Jumamosi katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika katika kituo cha treni katikati ya Kyiv, akiongeza kuwa alikuwa “haogopi kukutana” na Putin kama hilo litapelekea kufikia amani kati ya nchi hizo mbili.

XS
SM
MD
LG