Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Desemba 26, 2024 Local time: 13:38

Ukraine yajaribu kuwaondoa wanawake, watoto na wazee kutoka mji wa Mariupol


Moshi uliotanda katika kiwanda cha Chuma cha Azovstal katika mgogoro wa Ukraine-Russia katika mji wa bandari kusini mwa Mariupol, Ukraine April 21, 2022. REUTERS/Alexander Ermochenko
Moshi uliotanda katika kiwanda cha Chuma cha Azovstal katika mgogoro wa Ukraine-Russia katika mji wa bandari kusini mwa Mariupol, Ukraine April 21, 2022. REUTERS/Alexander Ermochenko

Ukraine itajaribu kuwaondoa watu Jumamosi kutoka mji wa bandari uliozingirwa wa Mariupol.

Naibu Waziri Mkuu wa Ukraine Iryna Vereshchuk amesema kupitia ujumbe wa Telegram kuwa mamlaka itajaribu kuwaondoa wanawake, watoto na wazee kutoka katika mji ambao majeshi ya Russia wamezuia juhudi za awali za kuwaondoa.

Si rahisi kwamba njia za kibinadamu kwa umma zitakuwa wazi Jumamosi, mamlaka imesema. Maafisa wanakadira kuwa kuna watu wengi wanaofikia 100,000 waliobakia Mariupol.

Wakati huo huo, Ufaransa na Ujerumani ambao waliwahi kuipatia silaha Russia pamoka na vifaa vya kijeshi venye thamani ya dola milioni 300 huenda “vinatumika huko Ukraine,” kulingana na ripoti maalum, inayotokana na takwimu za Tume ya Ulaya, zilizochapishwa katika gazeti ya The Telegraph, la Uingereza.

Gazeti hilo limeripoti kuwa vifaa hivyo vilikuwa vimepelekwa, licha ya marufuku pana ya silaha ya Umoja wa Ulaya kuhusu kuipatia silaha Russia ambayo iliwekwa kufuatia kujiingiza kimabavu kwa Russia huko Crimea mwaka 2014.

Ujerumani imetetea mauzo hayo, ikisema kuwa vifaa hivyo vilikuwa na matumizi ya aina mbili na kwamba Russia walisema vilikuwa vinahitajika kwa ajili ya raia na siyo matumizi ya kijeshi.

Gazeti hilo limesema vifaa vilivyopelekwa
Russia ni pamoja na “mabomu, roketi, makombora na bunduki.” Makampuni ya Ufaransa pia yalipeleka “Kamera kwa ajili ya vifaru zaidi ya 1000 vya Russia na pia mifumo ya uongozaji safari kwa ajili ya ndege za kivita na helikopta za mashambulizi,” gazeti la Telegraph limeripoti.

Kiasi cha nchi 10 wanachama wa EU wamepeleka takriban vifaa vya kijeshi venye thamani ya karibu dola milioni 380 kwa Russia, gazeti la The Telegraph limeripoti, na asilimia 78 ya jumla ya idadi hiyo vikitokea kwenye kampuni za Ufaransa na Ujerumani.

Nchi nyingine za Ulaya zilizoiuzia silaha Russia ni pamoja na Austria, Uingereza, Bulgaria, Jamhuri ya Czech na Italia, kulingana na The Telegraph.

Cristian Terhes, mbunge wa Romania katika Bunge la Ulaya aliwapa gazeti la The Telegraph tathmini ya EU juu ya uchunguzi huo unaoangazia nchi zipi zilizoiuzia Russia vifaa vya kijeshi.

Rais Volodymyr Zelenskyy (Ukrainian Presidential Press Office via AP)
Rais Volodymyr Zelenskyy (Ukrainian Presidential Press Office via AP)

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy Ijumaa alitumia maelezo ya Jenerali wa Russia kama ushahidi kwamba Moscow huenda itazivamia nchi nyingine iwapo itafanikiwa huko Ukraine. Jenerali huyo alisema Russia ina lengo la kukamata eneo lote la kusini na mashariki mwa Ukraine na kuziunganisha jimbo lililojitenga katika nchi jirani ya Moldova.

"Huu ni uthibitisho wa kile ambacho tayari nimekisema mara kadhaa: Uvamizi wa Russia nchini Ukraine ulikuwa ni mwanzo tu,” Zelenskyy alisema katika hotuba yake Ijumaa jioni.

XS
SM
MD
LG