Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Novemba 24, 2024 Local time: 04:46

Marekani na Russia wabadilishana wafungwa


Mwanajeshi wa zamani wa Marekani Trevor Reed akishindikizwa kwenye ndege na maafisa wa Russia mjini Moscow, kama sehemu ya kubadilishana wafungwa kati ya Marekani na Russia, April 27, 2022. Picha ya Reuters
Mwanajeshi wa zamani wa Marekani Trevor Reed akishindikizwa kwenye ndege na maafisa wa Russia mjini Moscow, kama sehemu ya kubadilishana wafungwa kati ya Marekani na Russia, April 27, 2022. Picha ya Reuters

Marekani na Russia Jumatano wamebadilishana wafungwa licha ya uhusiano wao wenye mvutano mkali kutokana na vita vya Ukraine. Mwanajeshi wa zamani wa Marekani Trevor Reed ameachiliwa huru baada ya Marekani kumuachilia rubani wa Russia Konstantin Yaroshenko.

Ubadilishanaji huo sio sehemu ya mazungumzo pana ya kidiplomasia wala haubadili msimamo wa Marekani kuhusu vita vya Ukraine, maafisa wa Marekani wamesema.

Reed ambaye ni kutoka jimbo la Texas, alikuwa njiani kuungana tena na familia yake hapa Marekani, maafisa waandamizi wa utawala wa Biden wamesema, na kuongeza kuwa mwanaume huyo mwenye umri wa miaka 30 alikuwa katika hali nzuri.

“Leo tunamkaribisha nyumbani Reed na tunasherekea kurudi kwake katika familia yake ambayo ilikuwa inamkumbuka sana,” Rais Joe Biden amesema katika taarifa.

Reed alikutwa na hatia nchini Russia mwaka wa 2019 kwa kuhatarisha maisha ya maafisa wawili wa polisi “akiwa amelewa” alipokuwa ziarani mjini Moscow.

Marekani iliitaja kesi yake “kuwa igizo la upuuzi.”

Maafisa wa Marekani wamesema Biden alibadilisha hukumu ya Yaroshenko, rubani wa Russia ambaye alikamatwa na kikosi maalum cha Marekani nchini Liberia mwaka wa 2010 na kukutwa na hatia ya kula njama ya kusafirisha dawa ya kulevya aina ya cocaine hadi Marekani.

Ubadilishanaji wa wafungwa hao ulifanyika nchini Uturuki, Marekani imemshukuru mshirika wake huyo wa NATO kwa kufanikisha ubadilishanaji huo.

Biden na waziri wa mambo ya nje Antony Blinken wamesema wanafanya juhudi ili mmarekani mwingine mwanajeshi wa zamani anaeshikiliwa Russia, Paul Whelan aachiliwe huru.

XS
SM
MD
LG