Kura zilizohesabiwa ambazo ni asilimia 99 ya kura zilizopigwa mjini Ankara, inaonyesha kwamba Meya wa muungano wa vyama vya upinzani ameshinda kwa asilimia 50.89, huku chama chake Edoragn cha AKP kikipata asilimia 47.06.
Mjini Istanbul, wagombea wote wa vyama vikuu wamedai ushindi. chama cha AKP kimepata asilimia 48.7, huku upinzani ukiwa na asilimia 48.65.
Erdogan akubali kushindwa
Erdogan akizungumza mjini Istanbul na waandishi wa habari, amekubali kuwa chama chake kimepata pigo na kuahadi kuwa litakuwa ni somo kutokana na uchaguzi huu.
"Tulikuwa na ushindi kidogo na tumeshindwa katika sehemu nyingine," amesema. Erdogan ameahidi kuanzisha hatua za kuboresha uchumi ambao umedorora.
Uwezekano wa chama tawala kushindwa Ankara
Baadhi ya wachambuzi wanaona kitendo cha Erdogan kujizuia na matamko makali dhidi ya chama cha Upinzani cha CHP ikiwa ni dalili ya kukubali chama chake kuwa kimeshindwa katika mji mkuu wa Ankara.
Mansur Yavas, mgombea wa nafasi ya meya Ankara kutoka chama kikuu cha muungano wa upinzani inaonekana ataweka rikodi ya kihistoria katika ushindi usio kuwa wa kishindo wa upande wa upinzani.
Imetayarishwa na Mwandishi wetu, Washington, DC.