Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 09:57

Nini hatma ya mvutano wa Marekani na Uturuki?


Andrew Craig Brunson, mhubiri wa injili anayezuiliwa nyumbani mji wa Izmir, Uturuki, Julai 25, 2018.
Andrew Craig Brunson, mhubiri wa injili anayezuiliwa nyumbani mji wa Izmir, Uturuki, Julai 25, 2018.

Kuongezeka kwa mvutano kati ya Uturuki na Marekani kunapelekea kuwepo hisia kwamba Uturuki inapewa motisha zaidi kuimarisha uhusiano wake na Russia.

Maafisa wa ngazi ya juu wa Uturuki wamekutana na maafisa wenzao wa Russia na Iran Jumatatu katika hoteli ya Sochi sea resort nchini Russia ikiwa ni sehemu ya ushirikiano ulioko kati ya nchi hizo juu ya kutafuta ufumbuzi wa vita ya wenyewe kwa wenyewe inayoendelea nchini Syria.

“Tunaweza kutafuta njia yetu wenyewe,” vyombo vya habari Jumapili vimemnukuu Rais Recep Tayyip Erdogan akisema hayo. “Marekani inaweza kupoteza mshirika mwaminifu na muhimu,” ameongeza wakati akijibu vitishio vilivyotolewa na Marekani.

Katika wiki zilizopita, mvutano umeendelea kuongezeka kati ya Uturuki na Marekani, wakati ambapo Rais Donald Trump akionya kuwa ataiwekea Uturuki “vikwazo vikali” iwapo Uturuki haitamwachia mchungaji wa Marekani, Andrew Brunson, toka kizuizini.

Brunson yuko kizuizini nyumbani kwa tuhuma za ugaidi ambazo Washington inazipinga kuwa hazina msingi “wowote.” Ankara inasema suala hilo ni jukumu la mahakama.

Wakati huo huo Russia inaendelea kufanikiwa kuwa karibu zaidi na Uturuki.

“Haya ni mahusiano ya karibu zaidi ambayo yametokea katika historia ya jamhuri ya Uturuki,” amesema mwanadiplomasia wa ngazi ya juu Aydin Selcen, ambaye aliwahi kufanya kazi Washington na Mashariki ya Kati.

Nchi hizi mbili zimeimarisha uhusiano wa ushirikiano wao kutokana na vita vya wenyewe kwa wenye vinavyoendelea Syria na pia upande wa biashara.

XS
SM
MD
LG