Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Desemba 24, 2024 Local time: 19:04

Maafisa Polisi wa Uturuki washtakiwa kwa jaribio la mapinduzi


Mwanajeshi akiwa nje ya eneo la mahakama ambako maafisa 29 wa zamani wa polisi wameshtakiwa kwa jaribio la mapinduzi
Mwanajeshi akiwa nje ya eneo la mahakama ambako maafisa 29 wa zamani wa polisi wameshtakiwa kwa jaribio la mapinduzi

Serikali ya Uturuki inaendelea kumlaumuFethullah Gulen kwa kuhusika na mauaji ya balozi wa Russia nchini Uturuki mwezi huu.

Uturuki imeanza kusikiliza kesi 29 za maafisa wa polisi wanaoshtakiwa kwa kusaidia mapinduzi yaliyshindikana na kusababisha vifo vya watu 270 na kupelekea serikali kuanzisha msako mkubwa.

Waendesha mashtaka wamesema wale wanaokabiliwa na tuhuma hizo za kusaidia mapinduzi hawakuwajibika pale walipotakiwa kuilinda Ikulu ya Rais Recep Tayyip Erdogan.

Maafisa 21 kati ya wale waliokamatwa wanakabiliwa na kifungo cha maisha iwapo watakutwa na hatia ya jaribio la mapinduzi, wakati wengine waliobaki wanakabiliwa na adhabu zisizo pungua kifungo cha miaka 15 kwa kuwa wanachama wa kikundi cha kigaidi.

Uturuki imeendelea kumlaumu Fethullah Gulen kufuatia jaribio hilo la mapinduzi, kiongozi wa kidini anayeishi Marekani ambaye amekanusha kuhusika na jaribio hilo.

Tangu Julai, serikali ya Uturuki imewakamata watu 40,000 na kuwafukuza kazi watu zaidi ya 100,000 wakiwemo watendaji wa serikali, waalimu, majaji na wengine wanaosadikiwa kuwa na mahusiano na Gulen au kujihusisha na hujuma hiyo. Hatua zaidi zimechukuliwa na serikali kusitisha shughuli zote za asasi za kijamii.

Wapinzani, wakiwemo serikali za magharibi na mashirika ya haki za binadamu, wanalalamika kwamba ulipizaji kisasi umevuka mipaka na sasa siyo tu wale wanaoshukiwa kushiriki katika mapinduzi ndio wanalengwa lakini hali hii inalenga taasisi ambazo zinapinga sera za Erdogan.

Serikali ya Uturuki imemlaumu Gulen kwa kuhusika na mauaji ya balozi wa Russia nchini Uturuki mwezi huu wakati alipokuwa anahudhuria maonyesho ya sanaa mjini Ankara. Serikali ya Russia imesema inasubiri mpaka tume ya pamoja ya uchunguzi itakapohitimisha uchunguzi wake kabla ya kulaumu upande wowote.

XS
SM
MD
LG