Rais wa Marekani Donald Trump ametishia kuiwekea Uturuki vikwazo kama sehemu ya kampeni ya kutaka mhubiri huyo aachiliwe huru.
Brunson amekuwa akizuiliwa gerezani kwa mda wa miezi 21 sasa kwa madai ya kusaidia kundi linaloongozwa na mhubiri wa kiislamu wa kituruki aliye uhamishoni Marekani Fethullag Gulen katika jaribio lililoshindwa la kumpindua rais Recepp Tayyip Edirgan.
Rais wa Marekani Donald Trump ametishia kuiwekea Uturuki vikwazo vikubwa iwapo haitamwachilia huru mhubiri raia wa Marekani ambaye amewekwa kizuizini nyumbani kwake nchini Uturuki.
Mgogoro huu wa kuzuiliwa raia wa Marekani umepelekea kuharibu uhusiano uliokuwepo kati ya washirika wa karibu wa muungano wa NATO.
Serikali ya Uturuki imeshikilia kuwa Brunson ana kesi ya kujibu kwa tuhuma za kusaidia mtandao ambao Uturuki inaulaumu kwa jaribio la kupindua serikali ya Rais Recep Tayyip Erdogan 2016, pamoja na kuhusika na kuwasaidia wapiganaji wa Kikurdi ambao wamepigwa marufuku kisheria.
Mchungaji huyo mwenye umri wa miaka 50, ambaye anakanusha tuhuma hizo, anaweza kukabiliwa na kifungo cha hadi miaka 35 jela iwapo atapatikana na makosa.
Rais Donald Trump wa Marekani mara kadhaa ameitaka Uturuki kumuachia Brunson.