Barr kutoa ufafanuzi kwa Seneti juu ya ripoti ya Mwendesha Mashtaka maalum

Mwanasheria Mkuu William Barr (kulia), Mwendesha Mashtaka Maalum Robert Mueller

Mwanasheria Mkuu wa Marekani William Barr anatarajiwa kujibu maswali ya wabunge Jumatano baada ya kutolewa kwa ripoti ya mwendesha mashitaka maalum Robert Mueller mwezi Aprili 2019.

Muelller alikuwa anachunguza taarifa juu ya Russia kuingilia kati uchaguzi mkuu wa Marekani mwaka 2016.

Bar atakutana na kamati ya sheria katika baraza la senate linaloongozwa na Warepublikan katika kikao kinachotarajiwa kuwa cha angalau masaa 3.

Bar atakutana na maswali kuhusu ripoti ya gazeti la Washington Post iliyotoka Jumanne usiku kwamba Mueller aliwasiliana na mwanasheria mkuu kwa njia ya simu na barua akimtaka ampe fursa ya kutoa maelezo juu ya ripoti iliyoandikwa na timu yake.

Badala yake Barr alitoa muhtasari wa taarifa yake mwenyewe kitu ambacho Mueller kwa uoni wake anasema haijatoa taswira ya kweli ya ripoti ya timu ya wachunguzi wake.

Imetayarishwa na Mwandishi wetu, Washington, DC.