Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Novemba 27, 2024 Local time: 13:38

Zimbabwe: Harare yakabiliwa na changamoto kubwa ya usambazaji maji


Women fetch water from a stream after Cyclone Idai in Chipinge, Zimbabwe, March 25,2019. REUTERS/Philimon Bulawayo
Women fetch water from a stream after Cyclone Idai in Chipinge, Zimbabwe, March 25,2019. REUTERS/Philimon Bulawayo

Mji mkuu wa Zimbabwe, Harare, una idadi kubwa ya watu na hivyo usambazaji maji umekuwa ni changamoto kubwa na hivyo mzigo wa kutafuta maji unawaangukia wanawake.

Usambazaji umeathiriwa na miundo mbinu ya siku nyingi ambayo inaweza kusababisha maji kuchafuka na malumbano ya ndani ya kisiasa nayo pia yanazuia maboresho.

Mzigo wa kupata maji safi mara nyingi unawaangukia wanawake kama anavyoripoti Keith Baptist kutoka Harare.

Marjorie Sande anasimamia kisima katika eneo la Mbare, sehemu maskini na yenye msongamano mkubwa katika vitongoji vya mji mkuu wa Zimbabwe, Harare.

Sehemu kama hiyo inapunguza umbali za kupata maji safi – shukran kwa eneo la mjini ambalo kwa miaka mingi lilikuwa na matatizo ya miaka mingi kupata fursa kama hiyo.

Marjorie Sande, Meneja wa Kituo cha Mbare: “Watu wengi kwa hakika wanapendelea kutumia pampu za kizamani, kinyume na maji ya bomba kutoka kwenye manispaa ya mji.”

Ujirani maskini unabeba mzigo wa uhaba wa maji huku wakazi mara kwa mara wakigeukia vyanzo vya umma kupata maji ya bure au ya gharama nafuu.

Meya wa Harare, Jacob Mafume anasema haifadhi ya eneo hilo, ilijenwa katika miaka ya 1950 lakini hivi sasa haiwezi kukidhi mahitaji ya jamii.

Jacob Mafume, Meya wa Harare: “Ziwa limetengenezwa kwa ajili ya watu laki tano na idadi kubwa ya watu mjini Harare hivi sasa imefikia milioni tatu. Kwahiyo, mahitaji yamevuka usambazaji.”

Mwanamke akiemea kuni katika mitaa ya Harare, Zimbabwe, March 2, 2021.
Mwanamke akiemea kuni katika mitaa ya Harare, Zimbabwe, March 2, 2021.

Rais Emerson Mnangagwa alizindua mpango wa visima vya maji mwanzoni mwa mwaka huu wa 2022 ili kuboresha fursa ya upatikanaji wa maji nchini Zimbabwe. Hii inatokana na juhudi za muda mrefu za wenyeweji na mashirika ya kimataifa ya misaada katika kutoa maji kwa umma. UNICEF inapanga kupeleka mashine za maji ambazo Sande watamuda kuzitumia.

Lakini wanawake ambao wanafika hapa wanasema wananyanyaswa na mara nyingine wanashambuliwa kimwili.

Baadhi ya wanaruka kwenye foleni ya kupata maji. Wengine ambao wanaitwa “wakuu wa vituo vya ugavi maji” – kinyume cha sheria wanachukua uongozi kwenye vituo vya maji na kutaka kuheshimiwa, fedha taslimu au upendeleo wa kingono kwa fursa ya kupatamaji.

Marjorie Sande, Meneja wa Kituo cha Mbare: “Wakati ambapo wanawake kwa kawaida wanapanga foleni mapema sana kwa ajili ya kile ambacho tunaweza kupata muda wa kutosha kuwatayarisha watoto wetu kwenda shule. Lakini wakati wanaume hawa wanapowasili, hawajali foleni wanakwenda moja kwa moja mbele na kuchota maji.”

Katika kliniki inayoshughulikia waathirika wa ubakaji kwenye hospitali ya Parirenyatwa mjini Harare wanasema kuna ripoti nyingi za watu kunyanyaswa au kushambuliwa wakati wakienda kuchota maji.

Tanaka Rwizi, umri miaka 16 mjamzito, akiwa nyumbani baada ya kuondolewa shuleni kwa kuwa mjamzito katika mji wa Mbare wenye umaskini, Harare, Zimbabwe, Saturday Nov. 13, 2021. (AP Photo/Tsvangirayi Mukwazhi)
Tanaka Rwizi, umri miaka 16 mjamzito, akiwa nyumbani baada ya kuondolewa shuleni kwa kuwa mjamzito katika mji wa Mbare wenye umaskini, Harare, Zimbabwe, Saturday Nov. 13, 2021. (AP Photo/Tsvangirayi Mukwazhi)

Trevor Nyakudya, afisa katika kliniki hiyo anaelezea zaidi.

Nyakudya anasema: “Hili shambulizi la ngono lililofanyika lina mkanganyiko.. inaweza kuwa ni hila kama “unataka maji, unahitaji kutoa aina fulani ya huduma ya ngono.”

Waathirika wengi hawajitokezi mbele kwasababu ya aibu, khofu, unyanyapaa au kwasababu hawajui hatua gani ya kuchukua, anasema Rutendo Mudayanhu.

Anafanyakazi katika program ya kuwawezesha wanawake – Shamwari Yemwanasikana ambayo kwa lugha ya kishona ina maana “marafiki wa mtoto msichana.”

Ili kusaidia, NGO hiyo pia imeandikisha wanaume wa kujitolea katika vituo vya maji.

Tapia Mujeni anawasaidia wakazi kupata maji anaelezea :“Lengo letu kuu ni kupambana na manyanyaso ya kijinsia, kwahiyo tayari tunawasaidia watu kwenye vitu vingi vya maji.”

Watetezi wanasema wanawake ni vyema wawe na sauti katika mpango, uawala na sehemu ambako kuna vituo vya maji pamoja na huduma za vyoo.

Febe Shoko mfanyakazi wa kijamii katika Water Alliance anaelezea zaidi.

Shoko, Afisa Ustawi wa Water Alliance anaeleza: “Kwa kweli tunataka suluhisho la kudumu ambako tunaweza kupata fursa ya maji kwenye mabomba yetu, kutoka majumbani mwetu ambako tunahisi tuko salama.

Imetayarishwa na mwandishi wetu, Khadija Riyami, Washington.

XS
SM
MD
LG